Sibishi kabisa kwa hili mkuu, nimezunguka sana mitandao lakini nimeamua kurudi Vodacom; nimerudi nyumbani.
Tigo nilikuwa naitumia Home Internet yao, lakini ipo very tempermental - mara moja inafanya kazi vizuri mara nyingine 4G inashida, mpaka uswitch to 3G ndio utapata atleast 1Mb/s. Mwisho wa siku nikachoka haya matatizo.
Nikanunua line ya Airtel, hapa ndipo nikabugi kabisa, mara mia Tigo; maana hawa jamaa ni headache hata kusteam video WhatsApp ni tatizo, wanakupa double bundle lakini wanafahamu fika kuwa huto zimaliza kwa amani. Nimebidi niiweke kwenye router nisiyoitumua idownload pole pole game zangu - maana piga ua hizo GB 88 walizonipa zitaisha tu.
View attachment 1671060