Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Sawa vinapatikana wapi na nani anaunganisha
Voda wenyewe ndio wanauza,mimi natumia kwenye router so waliniuzia hiyo sim card na kuniunga kwenye iko kifurushi,kwenye menu yao ya *149*03# utakikuta iko kifurushi kwenye internet then nenda kasi internet,ila nakushauri uende ofisini kwao wakuelekeze zaidi,ni unlimit kweli kwa elfu 50 nafanya fujo zote za internet kwa mwezi mzima,netflix,youtube n.k

20211229_122541.jpg
 
Voda wenyewe ndio wanauza,mimi natumia kwenye router so waliniuzia hiyo sim card na kuniunga kwenye iko kifurushi,kwenye menu yao ya *149*01# utakikuta iko kifurushi kwenye internet then nenda kasi internet,ila nakushauri uende ofisini kwao wakuelekeze zaidi,ni unlimit kweli kwa elfu 50 nafanya fujo zote za internet kwa mwezi mzima,netflix,youtube n.k

View attachment 2061523

Duuuuh safi hiyo kumbe hata Voda shop wanazo aiseee
 
Hii ni thread ya vifurushi ambavyo sio rasmi kama vya chuo au vifurushi maalum ambavyo vinatoa kiasi kikubwa cha internet, nitalist vifurushi ninavyovifahamu kama kuna wanaojua vyengine watasaidia

Tigo
Kwa Tigo bonyeza *147*00# kisha chagua size yako, unaweza kupata vifurushi vizuri, Ila njia hii sio reliable kwani vifurushi hivyo hubadilika kila Mara.


Vodacom
Vodacom angalia kwenye ya kwako tu, piga *149*03# kuangalia ofa.

Airtel
-Vifurushi vya chuo
Hawa jamaa wana vifurushi vizuri zaidi vya chuo hasa cha usiku ambacho unapata 10gb kwa sh 600, pia kipo cha kawaida unapata 2gb kwa 1000 na 1.2gb kwa sh600. Kuvipata unahitaji kununua vocha za chuo zinazopatikana vyuoni au kutumia airtel money *150*60# kisha uchague ofa kabambe nafkiri option ya 6.

Halotel
-Royal bundles pengine kifurushi kizuri zaidi kwa Sasa kinakupa dakika takriban 200 na Internet unlimited kwa 0.5mbps kwa mwezi mzima. Ni vyema kwenda ofisi za Halotel na kununua line ya Royal bundle, pia unaweza kukuunga kwa kubonyeza menu yao ya *148*66#

-Mega bundle kwa shilingi 10,000 Unapata GB 15 ambazo unatumia mb 500 kila siku kwa mwezi, kujiunga ni *150*88#, unakiunga na salio la halopesa.

-Kifurushi Cha usiku kwa 1000 unapata Internet unlimited, kizuri kwa ajili ya kudownload files kubwa Kama games na movies. Kujiunga *148*66# kisha vifurushi maalum (ya kwako tu)

vifurushi vya 4G kuendana na line zao mpya za 4G,
1000 unapata GB 1 kwa siku
5000 unapata GB 7 kwa wiki
10,000 unapata GB 10 kwa mwezi.


TTCL
-bandika bandua ni vifurushi vizuri kwa matumizi makubwa Kama kuangalia Netflix, zipo option Kama
-1000 GB 4 kwa siku (Mb 500 mchana 3.5GB usiku)
-2500 GB 10 kwa siku
-5000 GB 8 kwa wiki (3gb mchana na 5GB usiku)
Uzuri wake ni kwamba GB za usiku zinaanza saa 2 usiku muda mzuri ambao watu wanaangalia movies baada ya kutoka makazini.

-Toboa Night navyo ni vifurushi vizuri vya usiku in case Halotel kwako inasumbua ama Haina speed, kwa 500 unapata GB 2 na 1000 unapata GB 10.

Vyote toboa na bandika bandua unajiunga kwa kubonyeza *148*30# kisha TTCL bundles.

-Ofa maalum, pia TTCL Wana ofa mbalimbali Kama vile za sabasaba, nanenane etc ambazo wanazieka kwenye option ya vifurushi maalum,
Mkuu kuna mtu kaniambia Voda wana unlimited kwa mwezi ukitoa TZS 50,000/= basi utaona hadi Netflix bila kukwama au kuisha kwa mwezi mzima.
 
Mkuu kuna mtu kaniambia Voda wana unlimited kwa mwezi ukitoa TZS 50,000/= basi utaona hadi Netflix bila kukwama au kuisha kwa mwezi mzima.
Mkuu ni kile kifurushi cha 50,000 unapata GB 30, zikiisha unaendelea kutumia internet ila kwa speed ndogo,

Kwa 500kbps unaangalia netflix ila quality ndogo kabisa, kama ni Netflix kwenye TV huta enjoy angalau ukiangalia kwa simu inavumilika.

Ttcl kwako haijafika?
 
Mkuu fafanua uweke wazi watu wanataka huduma kama hizi ila huwashawishi coz kila anaeuliza una mwambia aje pm haya mambo ya njoo pm huwa watu wanayaogopa mkuu ila ukiweka hapa utawavutia na wengine wengine mfano mi nataka kujua ni free unlimited kwa mda gani na kwa tsh ngapi au kama kuna alieungwa na huyu mshikaji alete hapa mrejesho watu tupate huduma
Mimi ameniunga, nimekwenda pm japo nilikuwa na wasiwasi kupigwa lkn mwisho wa siku tulimalizana
 
Taperi huyu achananeni nae atawaliza kila mtu anamwambia njoo pm kuna nn cha ajabu huko pm kama sio kuibiana na kutapeliana, kama ni uongo kuwa sio taper wajitokeze hata watu wa3 watoe ushuhuda kama wamepata huduma kwa huju jamaa mzurulaji, kama unatoa huduma ya kweli basi unajikosesha hera mwenyewe unga hata watu 2 tu kisha waje hapa watoe ushuhuda na uone utakavo piga hera watu watakufata uwaunge mpaka utawakimbia mwenyewe kwa wingi wao.. Lakin bra bra nyingi hamna kitu.
Mimi nilijitoa akaniunga, japokuwa nilikuwa na hofu ya kupigwa lakini nikaenda, na ndio ninayotumia kwasasa hata kupost humu JF
 
Mkuu ni kile kifurushi cha 50,000 unapata GB 30, zikiisha unaendelea kutumia internet ila kwa speed ndogo,

Kwa 500kbps unaangalia netflix ila quality ndogo kabisa, kama ni Netflix kwenye TV huta enjoy angalau ukiangalia kwa simu inavumilika.

Ttcl kwako haijafika?
Nashukuru mkuu huku kwangu TTCL ni bure kabisa sijui kwanini, nipo mkoani,kijijini. Hata hivyo nashukuru.
 
Back
Top Bottom