Dedicated ina maanisha tu mda wote utapata 6mbps haimaanishi mkitumia watu wengi (Nyumba moja) speed haishuki.
Shared internet ina maanisha speed yako inaweza ikashuka ikiwa watu wengi wanatumia internet kwa wakati huo.
Chukulia mfano kampuni X imeleta Fiber 10Gbps capacity, wanaunga Vifurushi vya 10mbps kwenye Dedicated wataunga Exactly watu 1000 (1000x10mbps ni 10Gbps) ila kwenye Shared wanaweza wakaunga hata watu 5000 halafu mnagombania wenyewe hio bandwidth, assume siku kuna mechi kali kila mtu anatumia internet hapo ndio unaona speed inadrop toka 10mbps hadi 2mbps.
Pia mkuu most of time hizi internet za speed ndogo ni mtu wa kati, Mfano hio Microwave kuna possibility kubwa ni Vodacom supakasi, wapo pia wanaotumia za TTCL kisha wanauza rejareja.
TTCL tafuta fundi wa eneo husika, Sometime hakuna router tu hawaji kufungia watu, ukiongea nao unajua tatizo lipo wapi.