Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?

Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?

Habari zenu wana jamvi,

Katika pitapita huko mtandaoni nimeona taarifa ya operesheni anayoiendesha Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Mh Hassan Bomboko ya kutokomeza biashara ya ukahaba. Takribani miezi miwili amekuwa akiendesha kampeni ya kamata kamata wanawake anaodai ni madada poa na vilevile wanaume wanaodaiwa ni wanunuzi wa makahaba na kama hiyo haitoshi amekuwa akizigungia hadi bar mbalimbali zilizoko Ubungo na Sinza kwa madai ya kwamba zinawahifadhi makahaba.

Swali langu tu ,Je anatumia vigezo gani kuingilia faragha za watu ndani ya nyumba za kulaza wageni kama vile lodge ? Katika video iliyorushwa na Millard Ayo imeonesha akivamia lodge inayofahamika kama PR na kufungua vyumba vyote na kuwatoa watu katika faragha zao kwa madai kuwa ni makahaba na wanunuzi. Je hii ni sawa?

Pia amekuwa akizifungia lodges , je anataka wamiliki wa lodges wawe wanafanya kazi ya polisi kuhoji kazi ya kila mtu anayekwenda kuhitaji kupatiwa chumba cha kulala?

Vp ikiwa mtu amekwenda kupata faragha na mwenza wake katika hizo lodge halafu yeye anavamia na kuwaita watu ni makahaba na wanunuzi wa makahaba?

Kwa hali hii amefungia hadi Bar mbalimbali Sinza kwa kigezo cha kutopuga marufuku makahaba, je hawa wamiliki wanahusika vipi na masuala ya kufahamu kazi za watu?

Haoni kama anawatafutia hasara za kimapato hao wamiliki wa bar na lodges kutokana na kufungia biashara "halali" zinazoingizia Mapato serikali ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan.?

Chanzo: Millard AyoTv

View: https://m.youtube.com/watch?v=x4XCJyVLQ7E

Badala ya kuangaika na matokeo ya mfumo mbaya wa maisha na madhara ya hali ngumu ya maisha viongozi hawa wangekuwa wanajikita kwenye swala zima la kuifanya jamii iwe bora kuanzia mashuleni.
Tena kiongozi kijana kabisa huyu anatuangusha vijana wenzake..

kusanya hao dada poa waandikishe toa mwalimu wa ujasilia mali wa hapo manispaa awafundishe biashara then wape mtaji kupitia maendeleo ya jamii na wawafatilie kujua maendeleo yao kibiashara..

Huwezi ukamaliza biashara hii kwa zoezi la siku mbili au kuwa kamatakamata hapo anawasumbua wananchi mtaani..
 
Badala ya kuangaika na matokeo ya mfumo mbaya wa maisha na madhara ya hali ngumu ya maisha viongozi hawa wangekuwa wanajikita kwenye swala zima la kuifanya jamii iwe bora kuanzia mashuleni.
Tena kiongozi kijana kabisa huyu anatuangusha vijana wenzake..

kusanya hao dada poa waandikishe toa mwalimu wa ujasilia mali wa hapo manispaa awafundishe biashara then wape mtaji kupitia maendeleo ya jamii na wawafatilie kujua maendeleo yao kibiashara..
Suala kubwa hapa ni yeye kuingilia faragha za watu, kufungia lodges kwa madai ya kufanya biashara za kulaza makahaba bila ya vithibitisho vyovyote, pia anafungia bars wakati hao wote wanalipa kodi TRA na manispaa kufanya biashara. Sasa mwenye bar utamwambia kuwa aende akafukuze watu waliosimama barabarani kwa madai kuwa ni makahaba?
 
Huyu DC naye sijui ana bifu gani na hao MAKAHABA.....hivi kwa akili yake anadhani hii itasaidia??
Bora ajikite kwenye MAMBO YA MSINGI.
Alafu hao anaowakamata wakiwatuhumu kama makahaba,wakijiongeza kwenda mahakamani kufungua kesi ya udhalilishaji itakuwa KIZAAZAA kwa upande wake
 
Kama wana wanasheria wanafungua kesi na wanalipwa vizuri tu fidia
 
Kama wakifikira nje ya box kidogo tuu watagundua kwa kiasi kikubwa wao kama serikali wanachangia pakubwa vitu vya hovyo kama ukahaba kuendelea kuenea sana, kama wangekua wanasimamia vyema pesa za Watanganyika zikafanya kazi ipasavyo gharama za maisha zingekua chini na vitu kama ukahaba vingine vya hovyo isingekua jambo la kumfanya mkuu wa wilaya azunguke usiku kutafuta sifa kwamba anafanya kazi,
Hao makahaba wengi utakuta wanakodisha mbususu ili tuu wapate pesa ya kununua chakula na mahitaji ya kila siku, serikali ifikirie nje ya box
 
Viongozi mkurupuko akili kisoda, kuna Mambo ya msingi ya kuhangaika nayo, ila kuhangaika na ma barmaids ni ukosefu wa fikra
Mkuu kusheria mkuu wa Mko au Mkuu wa wilaya ana nguvu kusheria kufunga Buashara ilivyo funguliwa kwakufata sheria ?
 
Huyu ni mfano wa utaahira wa kuchanganya dini na siasa, yaani hapo limejiona ndio liislam safi eti.., akina Slaa na Makonda wanatafua migogoro lenyewe linaharibu uchumi na kuingilia faragha za watu..,

Viongozi wa kiislam ni laana kwenye nchi hii
 
Ila kuwa kiongozi Afrika raha sana. Unafanya utakacho na hakuna wakukufanya lolote.

Kwa nchi za wenzetu hilo ni bonge la lawsuit kwa wale waliotolewa vyumbani wakiwa na wenzi wao.

Ukute huyo mbwiga aligongewa mchepuko wake anaishia kuhamishia hasira zake zote kwa watu wengine.
 
Back
Top Bottom