Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Amekuwa akitunga mambo mepesi sana kuhusiana na matatizo yanayotokea kwenye masuala ya Chadema Arusha, Hitimisho linalotokana na uchunguzi wake ni la kusononesha mno! Ilipochomwa ofisi ya Chadema alikuja na majibu yasiyomridhisha hata mbumbumbu mzungu wa reli, jana Polisi wamevamia kituo cha Kampeni cha Mgombea ubunge wa Arusha mjini ndugu Lema, tuhuma zilizotolewa na RPC ukisikia unaweza kucheka na baadaye ukalia!
Kuna haja ya kubadili njia zinazotumika kuwapata askari wanaoteuliwa kuwa Makamanda wa mikoa ya kipolisi labda twaweza kuwapata wenye weledi .
Kuna haja ya kubadili njia zinazotumika kuwapata askari wanaoteuliwa kuwa Makamanda wa mikoa ya kipolisi labda twaweza kuwapata wenye weledi .