Tetesi: Vigogo watatu na maelfu ya wanachadema Kahama kutimkia CCM

Tetesi: Vigogo watatu na maelfu ya wanachadema Kahama kutimkia CCM

Taarifa nilizozipata kutoka chanzo changu cha uhakika kutoka mjini Kahama ni kuwa vigogo watatu toka CHADEMA watajisalimisha CCM wakati wa ziara ya mwenyekiti mpya wa CCM mjini humo.

Aidha licha ya vigogo hao ambao wote ni wale waliokihama chama hicho mwaka jana pia maelfu ya wanachadema wa kawaida wanatarajiwa kurejesha kadi zao na kujiunga CCM mbele ya mwenyekiti mpya.

Watu hao wanadai kuwa hawaoni sababu ya kuendelea kuwa wapinzani wakati wapinzani siku hizi wanakumbatia na kutetea ufisadi kwa kisingizio cha demokrasia.

Kwakweli ziara hii ni msiba kwa CHADEMA.

Naona yule mwanasiasa kijana machachali amewaingiza chaka sasa mmeamua kutoka kivingine.Chezea UKAWA wewe!
 
Hahahahaha hizi propaganda za kipuuzi mno, juzi hapa mlianzisha propaganda eti kabla ya tarehe 23 July 2016 kutatokea tukio kubwa sana la Vigogo wa UKAWA kuhamia CCM, waaapi labda kama walihamia ndotoni. too low for you
 
Haya mambo
Ng'ombe wanarudi zizini baada ya kwenda chadema na kutegemea maslahi wakaishia KUTAHIRIWA, sasa wanarudi zizini kuungana na wenzao waliokwepa tohara na wakaonekana mashujaa kwa kudumisha mila zao, uongo, chuki, dharau, kebehi. Wafike salama ila wamenyooshwa watakuwa na adabu.
Haya mambo ni kama basi,abiria wengine wanapanda na wengine wanashuka,sio issue wala sio news hata angerudi Lembeli.Watu wanatapatapa sana,Muheshimiwa Magufuli aliisha maliza huu mjadala wa ng'ombe waliokatika mikia hivyo tusijazejaze server bure
 
watakuwa hawana mikia ngoja ng'ombe waliobaki zizini wakawashangae
 
Hivi jamani CDM wamechangia madawati mangapi???
Jibu suala la sukari. Hivi umeshawahi kujiuliza kama hayo madawati yanawekwa kwenye vyumba gani? Ili madawati yawe na maana ni lazima wanafunzi wasizidi 45. Kama kuna wanafunzi 100 hayo madawati yanawekwa wapi? Aibu juu ya aibu. Mnapiga tu kelele lakini hamtaki kutumia akili. Ovyo kabisa.
 
Tehetehetehe. Wakirudi CCM watapewa muda wa kukiimarisha chama kutokana na athari walizozisababisha
mkuu,ukiona mtu ambaye mwenzie aliyehamia ccm amefananishwa na ng'ombe aliyekatwa mkia halafu naye anataka kwenda huko huko ujue huyo ni bongo lala!!
 
Hivi jamani CDM wamechangia madawati mangapi???



hata visima vya maji tukipewa msaada na wahisani viongozi wa ccm husema serikali ya mapinduzi imejenga wakat ni cha msaada wa bank ya dunia pesa za miradi hiyo huliwa hapa tunakuja suala la madawati hukuona wazazi walivyojitokeza kuchangia madawati? wakuu wa mikoa wanaongea ccm imetoa madawati heshimu michango ya watanzania uongo wenu pekeni lumumba au diamond yale madawati mia sita aliyotoa ni mwenyekiti wa ccm yule?
 
Mtoa mada inaelekea umetoka usingizini na kama siyo hivyo basi unaumwa
 
Back
Top Bottom