viingilio vya vijiwe vya bodaboda hufika mpaka laki 8, hii ni sawa ?

viingilio vya vijiwe vya bodaboda hufika mpaka laki 8, hii ni sawa ?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
933
Reaction score
3,051
watu wengi hudhani wamemaliza wakishanunua pikipiki na kuisajili, wasilolijua kuna gharama ya ziada ya kuingia kwenye kijiwe cha boda boda.

mfano kwenye vijiwe vya stendi na sokoni ada zipo juu mno zinafikia mpaka laki 8, na hapo ubahatike kuwe na nafasi ya wazi maana kuna limit ya idadi ya pikipiki.

kuanzisha kijiwe karibu yao unatafuta vita ya wazi, sio rahisi.

Hii ni sawa ?
 
Tofauti na hesabu za watu wengi wanaponunua bodaboda wakidhani wamemaliza kila kitu wakishanunua pikipiki na kuisajili kuna kitu cha ziada kinaitwa ada ya kiingilio kwenye kijiwe cha boda boda.

Pesa ipo kwenye vijiwe vya stendi na sokoni, ada za huko zipo juu mno zinafikia mpaka laki 8.

Hii ni sawa ?
Namlipa nani na je ipo rasmi kisheria au ni ujanja ujanja wa watu wa mjini?
 
View attachment 3277233

Tofauti na hesabu za watu wengi wanaponunua bodaboda wakidhani wamemaliza kila kitu wakishanunua pikipiki na kuisajili kuna kitu cha ziada kinaitwa ada ya kiingilio kwenye kijiwe cha boda boda.

kwenye vijiwe vya stendi, sokoni ada zipo juu mno zinafikia mpaka laki 8.

Hii ni sawa ?
Ulimwengu wa sayansi na technologia wewe unawaza kukaa vijiweni?
 
Mara nyingi hivo vijiwe, kuna mwenyekiti wao ndie anachukua hizo hela na kugawa kwa aidha serikali na zingine wanagawana wao boda.
 
Ndio ni sawa takwambia kwanini ?

Vijiwe hivi / Vikundi ni kama Saccos / Vikoba / Vikundi vya kusaidiana ambavyo huwa wanachangishana kila mwezi ili mmoja wao akipata shida aweze kusaidiwa; Sasa wewe unaingia leo hii unakuta watu mfuko wao ushatuna una mamilioni wewe ukipata shida au wakipata shida watakua msaada kama mwenzao au itakuwaje ?

Nadhani issue ya maana zaidi ni kuhakikisha na kuangalia Sera za hii nchi ya Wachuuzi na Madalali kama bado wanahitaji pia Wanaendesha Boda juu ya Machinga....
 
Back
Top Bottom