viingilio vya vijiwe vya bodaboda hufika mpaka laki 8, hii ni sawa ?

viingilio vya vijiwe vya bodaboda hufika mpaka laki 8, hii ni sawa ?

Vipi kwenye vijiwe vilivyo karibu na mageti ya hospital, huwa bei ni gani?
 
Sijui kwa nn , ama sio dharau ! Kuna maneno aliyaongea Lema khs boda boda, bado namsapoti ile sio kazi ! Kifo nje nje, mda na dakika yoyote ile
 
Ndio ni sawa takwambia kwanini ?

Vijiwe hivi / Vikundi ni kama Saccos / Vikoba / Vikundi vya kusaidiana ambavyo huwa wanachangishana kila mwezi ili mmoja wao akipata shida aweze kusaidiwa; Sasa wewe unaingia leo hii unakuta watu mfuko wao ushatuna una mamilioni wewe ukipata shida au wakipata shida watakua msaada kama mwenzao au itakuwaje ?

Nadhani issue ya maana zaidi ni kuhakikisha na kuangalia Sera za hii nchi ya Wachuuzi na Madalali kama bado wanahitaji pia Wanaendesha Boda juu ya Machinga....
Yaani huu upumbavu na ujinga wa waswahili kuanzisha ushirika wa kusaidiana katika shida naona umeshamiri sana, utasikia eti ukipata msiba napewa kiasi flani ooh ulifika na mtoto, ooh wazazi........kwa nn msikae mkafikiria vitu vingine vyenye Tija mkasaidiana , sasa unapompa pesa mfiwa unakuwa umemsaidia nn??
 
Issue ya kwanini wanasaidiana hio ni topic tofauti, ila issue ya kuombwa laki nani au zaidi kwa mfuko ambayo una zaidi ya mamilioni nadhani ni fair game..., na sio msiba tu mtu kugongwa, kuharibikiwa na pikipiki mikopo ya kukoeshana kupeleka watoto shule na mambo yote kulingana na katiba yao..

By the way mfiwa kupewa pesa haujamsaidia ? Msaada ni nini kurudisha mfu ili awe hai ?!!!
 
Back
Top Bottom