mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Ilibainisha hayo jana bungeni ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake, taarifa hiyo ilisomwa na mjumbe Yahaya Masare kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati.
Masare, Mbunge wa Manyoni Magharibi, alisema JKT hupokea vijana ambao wamehitimu kidato cha sita ambao huripoti kambini kwa ajili ya mafunzo bila kujali hali ya afya zao, wote hujumuishwa kuhudhuria mafunzo hayo.
"Ingawa kabla ya kuanza mafunzo wote hulazimika kupimwa afya zao, wale ambao watagundulika kuwa wajawazito tu ndio hurejeshwa nyumbani," alifafanua.
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2021, JKT ilichukua vijana kwa mujibu wa sheria ambapo mwaka 2019 vijana 20,413; mwaka 2020 vijana 21,383 na mwaka 2021 vijana 25,503.
"Hali ya maambukizi kwa vijana waliokuwa kambini kwa mujibu wa sheria kwa miaka hiyo mitatu ni kama ifuatavyo.
"Mwaka 2019 kati ya vijana 20,413 waliopimwa, 60 walikutwa na maambuzi; mwaka 2020 kati ya vijana 21,383 waliopimwa, 45 walikutwa na maambukizi na mwaka 2021 kati ya vijana 25,503 waliopimwa, 42 walikutwa na maambukizi," alibainisha.
Alisema vijana wenye VVU kambini JKT wanapatiwa huduma mbalimbali kama vile ushauri nasaha na kuanzishiwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI (ARV).
"Pia hupatiwa vipimo muhimu kabla ya kuanza dawa na hata baada ya kuanza dawa vipimo kama vya figo (Renal function test), maini (Liver function test) na CD4 Count na Viral load (Wingi wa virusi kwenye damu) pamoja na kupimwa magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu (TB Screening)," alisema.
Mjumbe huyo pia alisema kuwa pamoja na huduma hizo zinazotolewa na JKT, kamati imebaini kuwa bado elimu kuhusu umuhimu wa kujua afya ni mdogo lakini pia fedha za utekelezaji wa afua hazitoshelezi mahitaji.
IPP Media