Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzangu,
Kwanza kabla ya yote napenda kutumia nafasi hii kuiombea nchi yangu amani, upendo, mshikamano, ushirikiano, maendeleo ya watu na vitu.
Ndugu yetu mh Lisu baada ya kuishi ulaya miaka miwili mitatu, na kupata watu wawili watatu wa kumlipia kodi ya nyumba na hela ya kula huko Ubelgiji. Sasa amerudi nyumbani na jeuri ya kutoheshimu maamuzi ya chama chake, pamoja na maono ya viongozi wake.
Ndugu Tundu aidha kwa kushikwa masikio au kutokutumia akili kufikiri kile anachosema, amekuwa akitumia majukwaa mbali mbali kuwashambulia viongozi wake na chama chake kwa kukubali maridhiano ambayo yanaonesha njia ya kuliponya taifa kutoka katika zile siasa za majitaka alizozizowea Lisu hadi katika siasa kistaarabu ambazo ndio alizozizowea Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho.
Sasa kwa vile Lisu anataka kupimishana ubavu na mwenyekiti wa chama ambacho ndio kilichomfanya leo afike hapo alipo, basi acha sasa na chama chenyewe kim punish kwa kumuacha azurure tu mwenyewe akibwabwaja huku na kule bila msaada wowote wa maana kutoka kamati ya chama na viongozi wa chama kwa ujumla.
Siku mwenyewe akijirudi na kulijua kosa lake na kutubu hata kimya kimya, chama kitamsamehe na kumpa support zote azitakazo.
Yeye kajifanya kupiga ngumi kwenye chongo za misumari afu anategemea watu wenye akili zetu tutamsaidia kulia. Lisu akumbushwe kwamba hata siku moja sikio haliwezi kuzidi kichwa.