Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Maji, sukari, ladha, caffeine n.k ni vitu vipo kwenye vinywaji vingi tu, ai energy drink pekee mi nachohitaji kuelimishwa kuna chemical zipi zenye kuharibu figo kwenye energy drinks? Au kama kuna wingi wa chemical flani waeleze kitaalamu.
Possible mkuu fahamu kwamba energy drinks zote zina kiwango cha juu sana cha caffeine ambayo inasababisha madhara kwa figo in a long run...pia zina sukari nyingi ambayo inaweza kusababisha obesity na matatizo mengine ambayo tafiti zinasema huenda matatizo hayo yakarudi kuathiri figo...lakini pia energy nyingi zina kemikali ambazo zikitumiwa kwa mfululizo wa kipindi zinaweza leta shida kwa figo, kemikali hizo kwa mujibu wa mwandishi ni k.v. taurine, guarana na baadhi ya vitamini za kutengeneza pamoja na madini ambayo yanaweza kuwa na viambata-sumu, pia wanasema kemikali hizo zinaweza sababisha mawe ktk figo...mi nasoma tu hii makala kama mwananchi wataalamu wamo humu wanaweza kutuelekeza
 
At least hapa umeeleza mkuu, lakini kitaalamu zaidi inabidi waeleze milliliters kadhaa za energy drinks zina kiwango hiki cha caffeine na mwili wa mwanadamu unapaswa kupokea caffeine kiwango flani kwa mwezi au wiki n.k waeleze pia kiwango cha sukari kilichomo je kinazidi kiwango kinachohitajika katika mwili?

Kuhusu sukari hata hizi soda zina sukari nyingi.

Hii itasaidia watu watumie bidhaa hizo kwa vipimo maalumu.
Bado hawajaeleza kitaalamu zaidi.
 
Hapo sasa waje akina doktamathew tupate darasa
 
Sasa hivi kuna smart gin za 2k vijana wanachanganya na energy drinks, its terrible kwa kizazi hiki.
 
Ndo ukweli huo. Tafuta gazeti la Mwananchi la jana Machi 15, 2024 wameandika kwa kina sana...inaonekana unywaji pombe ni tatizo sana hasa kwa Vijana, ushahidi ni ukienda wikiendi Tabata, Kitambaa, Rainbow etc
Kwamba unawaamini Wananchi? Mtaani kwenu tafuta kama utapata aliyesababishiwa matatizo na energy drinks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…