Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Mishipa inaziba kwa sababu nyingi tu, ila alizotaja hapo ni za kawaida na hata kwenye soda tunazipata kasoro caffeine je na soda inapelekea matatizo ya moyo?

Hizi ni bra brah tu.
Mheshimiwa sema neno hapa Dkt. Gwajima D
Kwa mujibu wa Dokta Pedro wa Jakaya Kikwete Cardiac institute ni kwamba energy drinks zinasababisha mishipa ya moyo kuziba...anasema baadhi ya hizo energy drinks zina
  • maji
  • sukari
  • ladha
  • caffeine
  • mitishamba
  • tauline (amino acid)
  • protini
Na kemikali nyingine lukuki zenye athari kwenye mishipa ya moyo kwa sababu zinasupress mishipa ya moyo
 
Nimesoma gazeti la Mwananchi jana lenye kichwa cha Habari ukurasa wa mbele kisemacho
Pombe, 'energy drinks' zinavyomaliza vijana

Kwa mujibu wa hili gazeti wakinukuu wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma ni kwamba:-

1. Vijana Wanne hadi Tisa hufika Hospital hiyo kila wiki Figo zikishindwa kufanya kazi.

2. Watanzania 10 kati ya 100 wana tatizo la Figo

3. Wahanga ni vijana umri kati ya 24-40

4. Gharama za kusafisha Figo kwa mwaka ni wastani wa TZS 31,200,000 Hadi 46,800,000 bila kuweka gharama nyingine kv usafiri

5. Energy drinks ni disaster kwenye moyo kwa mujibu daktari bingwa wa JKCI.

6. Matumizi ya vinywaji hivi yanaathiri pakubwa viungo vitatu ambavyo ni
-Ini,
- Figo na
- Moyo.

7. Wahanga wakubwa ni vijana wa kiume.

MY TAKE:

Vijana acheni pombe, taifa linawategemea. Linda afya yako. Afya ni mtaji.
Pombe ya energy ipigwe marufuku
 
Mishipa inaziba kwa sababu nyingi tu, ila alizotaja hapo ni za kawaida na hata kwenye soda tunazipata kasoro caffeine je na soda inapelekea matatizo ya moyo?

Hizi ni bra brah tu.
Mheshimiwa sema neno hapa Dkt. Gwajima D
Ninyi wataalamu ndio tunawategemea mtuelimishe...Kuna wakati huwa mnatofautiana ktk maoni yenu hapo mnakuwa mnatutisha kidogo...ila mkitupa maelekezo mujarabu itafaa sana kulinda afya zetu...tuwekeni sawa kitaalamu.
 
Mishipa inaziba kwa sababu nyingi tu, ila alizotaja hapo ni za kawaida na hata kwenye soda tunazipata kasoro caffeine je na soda inapelekea matatizo ya moyo?

Hizi ni bra brah tu.
Mheshimiwa sema neno hapa Dkt. Gwajima D
 
Attachments

  • 17105946176138093766488111342086.jpg
    17105946176138093766488111342086.jpg
    1.2 MB · Views: 5
Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa mfano moyo, kiasukari presha na saratani yanakua na risk factors nyingi ikiwemo
👉Umri
👉mtindo wa maisha
👉Genetics
Na tunajua risk factors sio chanzo cha moja kwa moja bali ni mambo ambayo ukiyafanya yanaweza kukuelekea ukapata magonjwa hayo

Mtu anaweza asiwe na umri mkubwa na mtindo wake wa maisha ni wa kawaida sio sedentary lifestyle, anapiga zoezi vizuri lakini akapata kisukari akapata pia saratani na hata (cardiac diseases) juzi tu tumesolve kesi moja mtoto wa miaka miwili ana myocardial infraction. Ila anaendelea vema
Hapo kuna factor moja imebaki ambayo ni genetics.
Kuhusu energy drinks na kuleta magonjwa ya moyo probably inaweza sababisha lakini inaingia hapo kwenye mtindo wa maisha.
Energy drink ni kwaajili ya kupunguza fatigue ikiwa kuna ulazima wa kuendelea kufanya kazi na ingredient yake kubwa ni caffeine, ambayo pia unaipata kwenye kahawa na alkaloids zingine. (kwa waliokutana na pharmacognosy wataelewa nini namaanisha )ikitumiwa kiasi sidhani kama inaweza leta ugonjwa wa moyo, na tunajua too much is harmful.

Hapo juu nimeona kuna member anakunywa energy 6 kwa siku
Wanachuo wanakunywa energy na skonzi😂 hio ndio chai pia mtu anakunywa energy drink kisha anaenda kulala😂😂 for what?
Kwa staili hio tutapona kweli?
All in all too much is harmful

Dkt. Gwajima D
Dr Restart
DR Mambo Jambo
Dr am 4 real PhD

Mnaweza ongeza jambo hapa.
 
Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa mfano moyo, kiasukari presha na saratani yanakua na risk factors nyingi ikiwemo
👉Umri
👉mtindo wa maisha
👉Genetics
Na tunajua risk factors sio chanzo cha moja kwa moja bali ni mambo ambayo ukiyafanya yanaweza kukuelekea ukapata magonjwa hayo

Mtu anaweza asiwe na umri mkubwa na mtindo wake wa maisha ni wa kawaida sio sedentary lifestyle, anapiga zoezi vizuri lakini akapata kisukari akapata pia saratani na hata (cardiac diseases) juzi tu tumesolve kesi moja mtoto wa miaka miwili ana myocardial infraction. Ila anaendelea vema
Hapo kuna factor moja imebaki ambayo ni genetics.
Kuhusu energy drinks na kuleta magonjwa ya moyo probably inaweza sababisha lakini inaingia hapo kwenye mtindo wa maisha.
Energy drink ni kwaajili ya kupunguza fatigue ikiwa kuna ulazima wa kuendelea kufanya kazi na ingredient yake kubwa ni caffeine, ikitumiwa kiasi sidhani kama inaweza leta ugonjwa wa moyo, na tunajua too much is harmful.

Hapo juu nimeona kuna member anakunywa energy 6 kwa siku
Wanachuo wanakunywa energy na skonzi😂 hio ndio chai pia mtu anakunywa energy drink kisha anaenda kulala😂😂 for what?
Kwa staili hio tutapona kweli?
All in all too much is harmful

Dkt. Gwajima D
Dr Restart
DR Mambo Jambo
Dr am 4 real PhD

Mnaweza ongeza jambo hapa.
Asante sana 🙏🏾 daktari kwa ufafanuzi mujarab
 
Back
Top Bottom