Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Aisee Mimi bila Energy drinks sijisikii vizuri kabisaaa, 2014 nilikuwa nakunywa mpaka 6 per day lakini Sasa hivi asubuhi kabla sijala chochote lazima ninywe moja baridiii sana ndio nitafute chai Sasa. 🤣🤣🤣
😂😂😂au we ndo jirani yangu mtaani hapa maana story kama ya jirani yangu bila energy hataboi😂😂
 
Sio wewe ila kuna jirani hap saa 12 au saa 1 hivi utamuona na energy saa 3, saa 6 saa 8 na jioni bila kusahau usiku kwa siku anatembeza energy kama 5 au 6 ni sheria hiyoo😂😂 mo energy
Hiyo Mimi ilikuwaga miaka ya 2014, Mo Eneji nilikuwa nazinywa mpaka 6 au 7 sometimes mpaka Mangi alikuwa anakataa kuniuzia naenda duka jingine
 
Serikali ipige marufuku hizi energy drinks hasa za kwenye chupa za plastic maana zinauzwa mno bei rahisi.

Kama kuna ulazima ziwepo basi ziwepacked kwenye kopo za Alluminium na moja iuzwe 6,000 ili kuthibiti unywaji holela.

Kama pombe za karatasi za viroba zilipigwa marufuku, Serikali inashindwa nini kupiga marufuku huu ulevi wa energy drink ili kuokoa nguvu kazi ya nchi na kupunguza mzigo mkubwa kwa sekta ya afya?
Kwanza chupa zinachafua mazingira sababu wale waokota chupa hawana muda nazo. Nilishapandisha thread humu uchafuzi wake wa mazingira lakini hamna aliyechangia. Ile thread ilikufa kifo Cha mende
 
Aisee Mimi bila Energy drinks sijisikii vizuri kabisaaa, 2014 nilikuwa nakunywa mpaka 6 per day lakini Sasa hivi asubuhi kabla sijala chochote lazima ninywe moja baridiii sana ndio nitafute chai Sasa. 🤣🤣🤣
Energy drinks ukiizoea ina arosto kama cocaine, jitahidi kupunguza angalau moja kwa siku then taratibu una skip siku bila kutumia, Sikh mbili, tatu, wiki then uachane Nazo, mbaya zaidi wanywaji wa pombe Kali wanao miz na energy every single day baada ya miaka 5 watahitaji mil 32 za kujitibu figo kila mwaka au mil 300 kufanya replacement ya figo nyingine,so bro manyanza take care.
 
Watoe maelezo kitaalamu hizo energy drink zina chemical zipi ndani yake zinaopelekea kuharibu figo, sio kusema tu energy drinks zinaharibu figo.
Hii itasaidia sana watu wapate uelewa kwa upana zaidi.
Dr. Janabi amepiga kelele umuhimu wa kula vizuri uliona watu wanavyomnanga? Watz hata uwape maelezo na tafiti zote wasipokunanga watakuangalia tu... Ukitaka kuthibitisha angalia wenzako wanavyojibu kwenye huu uzi
 
Back
Top Bottom