Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Pia huwa nashangaa vijijini kuna vibabu toka tunakua mpaka now tunazeeka vinakunywa gongo na hatujawai kusikia hizi case za figo, ini wapo na wanadunda, Mimi nadhani hizo kemikali wanazoweka ndo zinaleta shida.
Yes wazungu kwenye pharmacetical industries ndio wanaoleta shida ili wauze dawa zao lazima watutie magonjwa
 
Dr. Janabi amepiga kelele umuhimu wa kula vizuri uliona watu wanavyomnanga? Watz hata uwape maelezo na tafiti zote wasipokunanga watakuangalia tu... Ukitaka kuthibitisha angalia wenzako wanavyojibu kwenye huu uzi
Lakini ni vyema watoe maelezo ya kitaalamu zaidi, si kila mmoja atakubali au kukuunga mkono, ni asili ya binadamu, mambo ya kiafya yaelezwe kitaalamu zaidi, waingie maabara wafanye tafiti waje na maelezo yanayojitosheleza kwingine ni uswahili tu.

Mfano kwenye hao wagonjwa wa figo wame conclude vipi kwamba chanzo chao kuugua ni energy drinks, je waliwauliza? Je miongoni mwao ni wangapi wanatumia energy? Kiasi gani kwa siku?

Lazima waje na taarifa zilizoshiba, bongo ubabaishaji mwingi.
 
Dr. Janabi amepiga kelele umuhimu wa kula vizuri uliona watu wanavyomnanga? Watz hata uwape maelezo na tafiti zote wasipokunanga watakuangalia tu... Ukitaka kuthibitisha angalia wenzako wanavyojibu kwenye huu uzi
Sasa janabi naye kazidi mambo ya kula karoti moja na glass tatu za maji asubuhi then saa kumi jioni ule slice moja na kipande cha tango baadae usiku ule kipande cha parachichi na wali uliopakuliwa kwenye kisosi nani ataweza?????
 
Janabi Sasa Anaipasua Nchi Amekuja Kwa Kasi Kama COVID 19 Vitisho Tu
Nadhani Baadaye Wakulima Watakosa Nguvu Sababu Ulaji Anaotaka Janabi
Watu Hawataweza Kubeba Hata Sindano Ikidondoka Chini, Watakuwa Hoi
 
Nyie hata mpewe maelezo yote mtaendelea tu na ratiba zenu. Haya mliambiwa mwanaume anatakiwa anywe bia mbili na nusu na mwanamke moja na nusu. Hiyo tu limewashinda, then mnataka research za energy drinks. Hata mkipewa mtasoma ?
 
Hawa vijana nilishawakanya kwa muda mrefu lakini hawanisikilizi. Sijui wanataka nini hasa.
Wanagida mipombe na mi energy kwa ujinga wao lakini wajishapata matatizo wanaanza kuilaumu serikali.
 
Waache ufisadi kwanza ndio watushauri...sgr wamemega mpka basi
 
Nyie hata mpewe maelezo yote mtaendelea tu na ratiba zenu. Haya mliambiwa mwanaume anatakiwa anywe bia mbili na nusu na mwanamke moja na nusu. Hiyo tu limewashinda, then mnataka research za energy drinks. Hata mkipewa mtasoma ?
Kuna ambao watafuata utaratibu kuna ambao hawatofuata.

Kwani hakuna watu wanakunywa beer mbili na hawaendelei?
Kwa kutoa maelezo ya kitaalamu kuna ambao yatawasaidia na kuna ambao ni vichwa ngumu lakini si kusema kwamba hata mkipewa maelezo hamtofuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…