Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
- Thread starter
- #21
Tunakumbushana tu. Nchi haiwezi kujengwa na wachache na vijana ndiyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele kufanya kazi na shughuli za uchumi.Take it easy bro....hakuna nchi ambayo watu wote wapo serious ndio maana nyie wasomi mmepewa jukumu la kufikiri kwa niaba ya nchi...
Umewasahau waliopo guest na bar..
Hii tabia ya kukaa vijiweni na hao unaosema wako bar na guest house sasa hivi ndiyo maana nchi ipo hapa ilipo maana vijana wanaomaliza shule wanakuta kaka na dada wanaamkia mpira, pombe na ngono siku za kazi.
Burudani ni muhimu lakini lazima kuwe na kipimo. Hata nchi zilizoendelea wapiga soga na pombe asubuhi wapo ila asilimia kubwa ya taifa watu wanafanya kazi na inawahamasisha vijana wao kufanya kazi kwa bidii ili kujitegemea na kumudu gharama za maisha. Hapa nchini kijana anajua hata asipofanya kazi anaweza kwenda kwa mjomba na akapewa chai.