Vijana asubuhi na mapema wako vijiweni kujadili mambo ya mpira, tutafika kweli?

Mkuu, vijana wa Tanzania wanapenda kufanya kazi.

Unaweza kusoma nyuzi kuhusu kazi za wiwandani hapa JF vijana wapo huko wanapambana hadi kwa ujira wa 4k kwa saa zaidi ya 11.

Vijana wa Tanzania mioyo yao inatoa damu.

Ukitazama zaidi utagundua ndiyo kundi linalolaumiwa kuanzia nyumbani hadi mitandaoni wanaonekana hawafai.

Lakini kwa hakika...

Wanapenda kufanya kazi na ndiyo maana unaweza kuona bodaboda, funzi ujenzi, tembea minadani kila sehemu wanapambana sana japo changamoto ni nyingi mno.

Ongea nao vizuri tu, hawa vijana wanapitia maisha magumu sana, usoni utaweza labda kuona huzuni zao lakini moyoni wanavuja damu.
 
Halafu hamjui tu, ila michongo mingi ipo vijiweni.
Sema 2 wakiwa wanabishana kuhusu mpira natamani hata nikawalambe kofi moja moja sio kwa makelele hayo ila kuna wakati wanakuwa wanaongea mambo ya muhimu unaweza ukatamani uwatoe ten ten
 
Jumanne, saa 3 hii tayari watu wamekaa vijiweni wanajadili Simba na Yanga. Hapa ndiyo nchi yetu ilipofikia, vijana kutumia muda mwingi kubishana kuhusu nani amesajiliwa na timu gani, analipwa kiasi gani wakati maisha yao yapo hohehahe.

Nchi ina hali mbaya sana kama kijana akitoka tu kuamka anawaza kuhusu maisha ya watu wengine na siyo ya kwake.

===
Pia soma;
Kwani vijana hao wakijadili mpira wakamaliza wanakuja kula kwako?

Msituletee vurugu za Kenya hapa, hizi nchi ziko tofauti sana. Jobless wa Tanzania anweza kuwa na maisha mazuri kuliko Mkenya aliyewjiriwa wa kipato cha chini. Wale watu hawana ardhi, ardhi imeshikwa na familia chache tu za mabilionea
 
Jumanne, saa 3 hii tayari watu wamekaa vijiweni wanajadili Simba na Yanga. Hapa ndiyo nchi yetu ilipofikia, vijana kutumia muda mwingi kubishana kuhusu nani amesajiliwa na timu gani, analipwa kiasi gani wakati maisha yao yapo hohehahe.

Nchi ina hali mbaya sana kama kijana akitoka tu kuamka anawaza kuhusu maisha ya watu wengine na siyo ya kwake.

===
Pia soma;
Wengine wanafanya kazi usiku..acha kukariri.
 
Sema 2 wakiwa wanabishana kuhusu mpira natamani hata nikawalambe kofi moja moja sio kwa makelele hayo ila kuna wakati wanakuwa wanaongea mambo ya muhimu unaweza ukatamani uwatoe ten ten
Pale sio sehemu ya kuwa serious all the time, wengi hawana mishe za day to day, kwahyo unakuta wapo to pass time siku iishe na bila kubishana na kupiga story za uongo na ukweli, Muda hausogei. Ila from time to time, Madini mengi yanatemwa vijiweni, michongo mingi ipo vijiweni, connection nyingi zipo vijiweni, ni akili ya mtu sasa kujiongeza akapambanie michongo akitoka kijiweni. Kama haujawahi kuishi maisha ya kimtaa mtaa, huwezi kabisa ukanielewa.
 
Sasa hivi nchi yetu imejiweka kwenye mtego kwa kutaka kuwa waandaji na wenyeji wa AFCON, matokeo yake mabilioni ya pesa yatatumika kujenga viwanja na miundombinu. Wakati bado kuna mtoto anakaa chini darasani, mama mjamzito anajifungulia nyumbani.

Sipingi ujio wa AFCON ila kama nchi tunapaswa kujiuliza vipaumbele vya taifa letu ni nini ili kuboresha maisha ya mtanzania: elimu na afya ni sekta zinazohitaji pesa nyingi ielekezwe huko.

Je, mpira unanyanyua maisha ya watanzania masikini kwa pamoja?
Upo sahihi sana mkuu... Umesema kiweledi na kiumakini kabisa,,, "kwamba nchi lazima izingatie vipaumbele muhimu" kwa hali ya uchumi wetu kiujumla sio mzuri sana.. Mpira iwe sehemu tu ya kuimarisha afya zetu kama michezo mwingine sio kutumia muda na pesa kiasi kila ilihali Haina faida yeyote kwa chumu...
 
Hiyo ni sehemu ndogo sana ya vijana wa kitanzania unayoizungumzia. Hayo yapo kwenye miji mikubwa tu, miji mingine yote vijana wapo kwenye kuchapa kazi.
Hata hao unaozungumzia ni wale ambao hawana kazi maalum.
 
Jumanne, saa 3 hii tayari watu wamekaa vijiweni wanajadili Simba na Yanga. Hapa ndiyo nchi yetu ilipofikia, vijana kutumia muda mwingi kubishana kuhusu nani amesajiliwa na timu gani, analipwa kiasi gani wakati maisha yao yapo hohehahe.

Nchi ina hali mbaya sana kama kijana akitoka tu kuamka anawaza kuhusu maisha ya watu wengine na siyo ya kwake.

===
Pia soma;
Wape michongo
 
Sasa hivi nchi yetu imejiweka kwenye mtego kwa kutaka kuwa waandaji na wenyeji wa AFCON, matokeo yake mabilioni ya pesa yatatumika kujenga viwanja na miundombinu. Wakati bado kuna mtoto anakaa chini darasani, mama mjamzito anajifungulia nyumbani.

Sipingi ujio wa AFCON ila kama nchi tunapaswa kujiuliza vipaumbele vya taifa letu ni nini ili kuboresha maisha ya mtanzania: elimu na afya ni sekta zinazohitaji pesa nyingi ielekezwe huko.

Je, mpira unanyanyua maisha ya watanzania masikini kwa pamoja?
Ukifafanya cost analysis utagundua kwa nchi masikini kuandaa hii michuano kuna hasara zaidi ya faida.
 
Back
Top Bottom