Vijana asubuhi na mapema wako vijiweni kujadili mambo ya mpira, tutafika kweli?

Mkuu, vijana wa Tanzania wanapenda kufanya kazi.

Unaweza kusoma nyuzi kuhusu kazi za wiwandani hapa JF vijana wapo huko wanapambana hadi kwa ujira wa 4k kwa saa zaidi ya 11.

Vijana wa Tanzania mioyo yao inatoa damu.

Ukitazama zaidi utagundua ndiyo kundi linalolaumiwa kuanzia nyumbani hadi mitandaoni wanaonekana hawafai.

Lakini kwa hakika...

Wanapenda kufanya kazi na ndiyo maana unaweza kuona bodaboda, funzi ujenzi, tembea minadani kila sehemu wanapambana sana japo changamoto ni nyingi mno.

Ongea nao vizuri tu, hawa vijana wanapitia maisha magumu sana, usoni utaweza labda kuona huzuni zao lakini moyoni wanavuja damu.
 
Halafu hamjui tu, ila michongo mingi ipo vijiweni.
Sema 2 wakiwa wanabishana kuhusu mpira natamani hata nikawalambe kofi moja moja sio kwa makelele hayo ila kuna wakati wanakuwa wanaongea mambo ya muhimu unaweza ukatamani uwatoe ten ten
 
Kwani vijana hao wakijadili mpira wakamaliza wanakuja kula kwako?

Msituletee vurugu za Kenya hapa, hizi nchi ziko tofauti sana. Jobless wa Tanzania anweza kuwa na maisha mazuri kuliko Mkenya aliyewjiriwa wa kipato cha chini. Wale watu hawana ardhi, ardhi imeshikwa na familia chache tu za mabilionea
 
Wengine wanafanya kazi usiku..acha kukariri.
 
Sema 2 wakiwa wanabishana kuhusu mpira natamani hata nikawalambe kofi moja moja sio kwa makelele hayo ila kuna wakati wanakuwa wanaongea mambo ya muhimu unaweza ukatamani uwatoe ten ten
Pale sio sehemu ya kuwa serious all the time, wengi hawana mishe za day to day, kwahyo unakuta wapo to pass time siku iishe na bila kubishana na kupiga story za uongo na ukweli, Muda hausogei. Ila from time to time, Madini mengi yanatemwa vijiweni, michongo mingi ipo vijiweni, connection nyingi zipo vijiweni, ni akili ya mtu sasa kujiongeza akapambanie michongo akitoka kijiweni. Kama haujawahi kuishi maisha ya kimtaa mtaa, huwezi kabisa ukanielewa.
 
Upo sahihi sana mkuu... Umesema kiweledi na kiumakini kabisa,,, "kwamba nchi lazima izingatie vipaumbele muhimu" kwa hali ya uchumi wetu kiujumla sio mzuri sana.. Mpira iwe sehemu tu ya kuimarisha afya zetu kama michezo mwingine sio kutumia muda na pesa kiasi kila ilihali Haina faida yeyote kwa chumu...
 
Hiyo ni sehemu ndogo sana ya vijana wa kitanzania unayoizungumzia. Hayo yapo kwenye miji mikubwa tu, miji mingine yote vijana wapo kwenye kuchapa kazi.
Hata hao unaozungumzia ni wale ambao hawana kazi maalum.
 
Wape michongo
 
Ukifafanya cost analysis utagundua kwa nchi masikini kuandaa hii michuano kuna hasara zaidi ya faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…