mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,718
- 7,784
Wana-JF, mimi nawasalimia. Kwa muda sana natafakari haya maisha ya hawa vijana hususani wa kitanzania, ambao wanakataa ndoa. Kwa tafiti zangu 'informal', nimebaini kuna tatizo kubwa sana linapelekea hili. Nalo si jingine, ni NJAA.
NI wazi, usipokula lishe bora, hata akili yako haifikiri vema, hali inayopelekea kulipuka lipuka na kuwa na hasira hasira, mtu wa shari shari, nk. Haya yote yanaletwa na njaa.
Ukishinda njaa toka asubuhi mpaka jioni, halafu ukaingia IG, TikTok and the like, na ukaona namna mabinti wabichi wazuri na wenye ngozi laini, namna wanavyo enjoy maisha, ni LAZIMA ukasirike tu automatically, hata kama hakuna alichokukera.
Ukishiba hali hiyo ya hasira inapungua automatically. Hata akili pia, inaanza kufanya kazi vema. Wakati mwingine unajutia mpaka maamuzi yako.
Watanzania wengi lishe ni MBOVU. Si kwa wanawake na si kwa wanaume. Lishe mbovu imefanya mpaka akili zimekuwa dormant. Hili limeathiri mpaka suala la kuoa, hasa kwa vijana wa kiume.
Asubuhi chai na mihogo miwili. Mchana bagia na energy, au sembe 1/4 na dagaa mchele, jioni mishkaki mitatu ya 200 na ugali wa sembe kama ngumi ya mtoto. Hapo siku imeisha. Nguvu za kiume zitatoka wapi? Akili yenye tija itatoka wapi? Ndiyo haya mauza uza tunayoyaona.
Siyo kwamba vijana hawataki kuoa, no, naamini wanataka ila suala ni KIPATO kinachofanya wawe na njaa. Maisha ya TZ hata chakula unachoona ni bei rahisi mikoani huko vijijini, mjini ni ghali.
Na ukifuatilia KATAA NDOA wengi ni vijana wanaoishi hapa hapa DSM, siyo mikoani.
Njaa! Njaa! Njaa! Ikiingia akilini ni LAZIMA uwe na roho ya kichawi ukisalimika kuwa mchawi kamili. Ukiona binti amependeza utachukia na kuapiza kutooa. Ukiona binti amejaliwa shape utachukia tu bila sababu na kuapia kutooa.
Njaa inawapiga vijana wa kike na wa kiume, ila wa kiume inaonesha kuwaathiri zaidi.
Njaa mbaya! Hakikisha unakula unashiba. Heri ukose bando lakini ule. Ni muhimu kwa sex drive yako na afya yako ya akili.
Vijana wakianza kula vema na kushiba, 90% ya hawa mabinti wote wataolewa. Jamani, kuleni.