mwanamke hata awe na sura nzuri au mbaya (kwa macho ya kibinadamu), unatakiwa kuoa yule anayekupenda zaidi ya wewe unavyompenda. usije kujaribu kuoa mwanamke ambaye wewe ndio unampenda zaidi, yeye anatakiwa kukupenda zaidi ya wewe unavyompenda. hapo utaishi vizuri. ila ukifanya hivyo vinginevyo nakuhakikishia lazima utakuja uchanike moyo siku moja. namshukuru Mungu nilifanikiwa kuoa mwanamke anayenipenda sana mimi kuliko vile mimi nilivyompenda, amenivumilia kwa mengi na mwisho wa siku tukaja kuendana, sasa tunapendana sawasawa na ndoa ni nzuri sana. kuna kaka yangu mmoja yeye alioa mwanamke mzuri sana na ana PHD, ila mwanamke hampendi sana, yeye brother ndio anampenda zaidi. ajabu yake, mwanamke pamoja na kwamba wamezaa watoto kadhaa, yupo tayari kuachana naye kama brother akiamua, na bro hayuko tayari kumwacha kwa jinsi anavyompenda hadi leo, hiyo sasa imekusa silaha/fimbo ya kumburuza, anamburuza bro apendavyo. kwasababo bro ndio anayejibembeleza kwake.