Vijana kachukueni Pasipoti zenu Uhamiaji mtawanyike Duniani; kusubiri ajira na uteuzi ni utumwa wa fikra

Passport watakwambia laki na 50.
Lakini kitambulisho Cha uraia unapewa bure[emoji856]
 
Kabla sijaona huu uzi nilikuwa naongea na jamaa yangu kwa njia ya simu yupo Tanga na Pangani anasimamia vyombo vya uvuvi vya jamaa zake,alichonieleza ni kuwa kule wakongo wanakwenda sana kuchukua samaki na dagaa,lakini hasa dagaa hawa baharini wanaitwa zanzibar fish kitu kama hicho anasema wanapakia tandamu kwa tandamu wanunuzi wakubwa ni wakongo.So nakubaliana na wewe nikiunganisha na taarifa aliyonipa jamaa yangu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Nipe hii connection mzee kwa mtaj Wa milion 1 nikiwa na gunia 7 naweza peleka huko Dagaa?
 
Ndiyo muende tatizo vijana sahv wanaishia kuongea tu

Ova
 
Passport watakwambia laki na 50.
Lakini kitambulisho Cha uraia unapewa bure[emoji856]

Hapo Kwenye Passport watakuambia Unasafiri?
Wanamaanisha Yaani Tayari unataka kwenda sehemu? Leta Uthibitisho!
Sio Eti Upewe halafu Uanze Kutafuta Ajira[emoji851][emoji851]Hawakupi Aisee tena wanasema Passport ni Mali ya Serikali.
Labda Sasa Hivi wawe wanebadilisha Huo Utaratibu!
 
Daaah, umeandika vizuri sana. Wazo hili lingefanyiwa kazi hakika lingeleta matokeo chanya. Ni kweli wapo vijana ambao ni smart sana kichwani lakini wamekosa mahali pa kuzitumia akili zao, ila zipo nchi zenye opportunities zinahitaji vijana kama hawa. Wakiwapata hawa wanawatumia ipasavyo na hivyo kuleta tija kwao na kwa vijana wenyewe. Kwa kuwa zipo nchi zinazohitaji rasilimali watu (Australia, Canada, nk), basi tuwe na idara inayoshughulikia masuala ya kuwapeleka vijana kufanya kazi nje kwa makubaliano maalumu (kati ya vijana na idara husika). Idara hii tuiite 'export brains'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…