Warioba ni kati ya watu wachache waliokuwa wanamrudisha Nyerere kwenye mstari.
Warioba alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria alikuwa anamfundisha Sheria Nyerere. Nyerere alitaka kufanya mambo nje ya sheria, Warioba akawa anamrudisha kwenye mstari.
Kuna mtu alishitakiwa na serikaki ya Nyerere, akashinda kesi, Nyerere akataka huyo mtu akamatwe tena ashitakiwe upya, Warioba akamwambia Nyerere huyu mtu kisheria hatakiwi kushitakiwa mara mbili kwa kosa moja, hiyo ni "double jeopardy". Akamkataza Nyerere kumshitaki
Nyerere akabaki kulalama lakini alishindwa kupangua hoja ya Warioba ya kisheria.
Hivi karibuni Warioba alieleza jinsi akivyosimamia sheria akipinga matakwa ya Sokoine ya kukamata na kushitaki watu kinyume na sheria, issue mpaka ikaoelekwa kwa Nyerere.
Katika watu waliokuwa wana uwezo mkubwa wa kubushana na Nyerere mmoja wao alikuwa Jiseph Sinde Warioba.
Warioba hajaanza kuwa hivyo anasema anachoona sawa keo, tangu kwenye serikali ya Nyerere alikuwa hivyo.
Na Nyerere alimoenda kwa sababu alimjua huyu jamaa si chawa.