Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Nimeshaona post kadhaa siku za nyuma vijana wa Kariakoo kupotea wakati nipo kwenye daladala ilibidi nimuulize jamaa mmoja kipindi cha nyuma kwanini vijana wa Kariakoo wanapotea sana, akasema Kariakoo kuna mambo mengi…aliishia hapo…

Ila kuna neno alisema kuna mchezo wa mali zinaibiwa mbali unapewa uuze, kuna mali kauli, cha msingi alikua anaongea mambo mengi.

Kama pia mnakumbuka wale vijana waliopotea wakati wa sherehe za eid wote ni vijana wa Kariakoo
Chai
 
Wengi wanaochangia wamemung'unya sana maneno kiasi asiyejua kinachoendelea hapati clue ya yanayotokea,vijana wanaopotea Kariakoo ni upande wa vitu kama simu laptop na tv na vitu mfanano wa hivyo pamoja na spare za magari.

Mimi nafanya biashara ya spare za magari,nyuma miaka saba nikiuza used kwanza Kariakoo kisha Ilala kule Lindi St so nikizungumza kwa upande huo nawajua vijana pamoja na watu wazima 11 wamepotea toka 2022 hadi leo hawajulikani walipo wa mwisho kwa upande huu walipotea wawili kwa pamoja mwaka jana mwezi wa tano na wote miaka ya nyuma wakati nafanya used walikuwa wanajihusisha sana na kununua vitu vilovyokuwa vikiibiwa kwenye magari ya watu wenyewe wakiita ”full",yaani gari inavunjwa kioo wanatoa lock wanachukua kuanzia dashboard show p/window switch radio side mirrors headrest nje wanang’oa taa zote bumpers nyuma na mbele kama mmiliki alisahau chochote cha thamani wanabeba so hawa jamaa walikuwa wanakaa pale mnada wa spare ulioungua moto nyuma ya Big Born p/station.

Jamaa walikuwa wanakula na askari wa Msimbazi na Central wakati fulani Mambosasa akiwa mkuu wa police Dar akalivalia njuga kwa kuwapa kitu kama offer (maana walikuwa wanajulikana ndiyo wanaodhamini biashara hiyo) kwamba kuanzia pale hawana kesi ila wakiri kuacha mara moja mchezo huo kwani option iliyokuwa ifanyike baada ya kudhihirika wanaendelea na kazi hiyo ni kupotezwa moja kwa moja na kwamba jeshi la polisi halitakuwa na muda wa kwenda kutoa maelezo mahakamani,kilichoendelea wanakijua wenyewe baadae walipovunja hicho kiapo ndiyo wakapotea.

Baada ya hii ambush ndiyo matokeo tunayoyaona sasa wizi ule umepungua kama siyo kuisha kabisa.
Mkuu umeeelezea vizuri sana Ila tunaomba uongezee nyama kidogo
 
Nimeshaona post kadhaa siku za nyuma vijana wa Kariakoo kupotea wakati nipo kwenye daladala ilibidi nimuulize jamaa mmoja kipindi cha nyuma kwanini vijana wa Kariakoo wanapotea sana, akasema Kariakoo kuna mambo mengi…aliishia hapo…

Ila kuna neno alisema kuna mchezo wa mali zinaibiwa mbali unapewa uuze, kuna mali kauli, cha msingi alikua anaongea mambo mengi.

Kama pia mnakumbuka wale vijana waliopotea wakati wa sherehe za eid wote ni vijana wa Kariakoo
Post imekamilika? au ndio umejoin leo? post za aina hii ni zinajaza server bure
 
Mkuu umeeelezea vizuri sana Ila tunaomba uongezee nyama kidogo
Mambo ni mengi sana yanayotokea hapa town lakini itoshe kusema kwamba kwa vyovyote ilivyo wanaoendesha hizo operations ni watu wanajua wanachokifanya hawabahatishi

Akija mtu anayejua yaliyokuwa yanaendelea pale Agrey ukamuuliza anaona mabadiliko gani baada ya ile crew ya vijana watano kupotea utashangaa anasema yapo mambo fulani yamebadilika sawa na kwangu upande wa spare za magari kumepoa nina muda mrefu sijamsikia mtu akitafuta vitu vyake vilivyoibwa.
 
Kwa hio mkuu kumbe kupotezwa kwao ndio kunajenga unafuu kwenu?
 
Kwa hio mkuu kumbe kupotezwa kwao ndio kunajenga unafuu kwenu?
Unafuu kwetu ukimaanisha kwenye biashara zetu?

Jibu ni hapana kwa sababu uwepo wao ulichangamsha biashara,mfano wewe gari yako ikiibwa spare utaingia sokoni kutafuta gari yako itembee so kama hukukutana na watu wanaoweza kukuuzia vitu vyako vile vile ulivyoibiwa (hao waliopotea ) utakuja kwangu nikuuzie so nakuwa nimeshafanya mzunguko.
 
Huwezi kuamini lakini pale Kariakoo kuna watu wamewaachia wake zao ujane na watoto kukosa baba,yupo jamaa yangu mmoja wa Kirangi akiitwa Shafii Irenda alipotea mwanae wa mwisho akiwa na wiki moja!

Hulazimishwi kuamini hata hivyo
Achana nae huyo asi kuumize kichwa sisi tunao shinda kariakoo 24/7/365 tunajua ni wakupuuzwa
 
Unafuu kwetu ukimaanisha kwenye biashara zetu?

Jibu ni hapana kwa sababu uwepo wao ulichangamsha biashara,mfano wewe gari yako ikiibwa spare utaingia sokoni kutafuta gari yako itembee so kama hukukutana na watu wanaoweza kukuuzia vitu vyako vile vile ulivyoibiwa (hao waliopotea ) utakuja kwangu nikuuzie so nakuwa nimeshafanya mzunguko.
Duuuh kwa hio walikua na faida kwenu pia
 
Back
Top Bottom