Ejolisi
Member
- Aug 26, 2022
- 57
- 87
Wazo hili nimelipata baada ya kupata maoni tofauti tofauti kutoka kwa baadhi ya vijana wa kitanzania tena wasomi kuhusu mchango wao katika siasa na hali halisi iliyoko kwa sasa.
Inasikitisha kuona kwamba hata wenye elimu na mwanga hawana muda wala uelewa wowote, wenye chachu na hamasa ya masuala ya uongozi na utawala ni wachache sana. Wengi wanadai kwamba hawana haja ya kujua siasa na kusahau kuwa siasa ndio inayotoa tafsiri ya mifumo yote ya nchi na ni kwa namna gani yatekelezwe.
Mabadiliko na maendeleo yanaletwa na watu wanaojua nini kinaendelea kwenye nchi, mifumo imekaaje, wapi pamepwaya. Vijana suala la kusema siasa haituhusu ni kwamba inatuhusu sana tena hari hii ipandikizwe mpaka kwa watoto.