Pre GE2025 Vijana kumchukulia Fomu ya Urais Rais Samia 2025

Pre GE2025 Vijana kumchukulia Fomu ya Urais Rais Samia 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika kumekucha,kumepambazuka Tanzania. Bendera imepandishwa,imepandishwa na vijana. Ni bendera ya upendo ,upendo kwa Rais samia kipenzi cha vijana aliyeleta na kuinua matumaini katika mioyo ya vijana,baada ya kutoa maelfu ya ajira kwa vijana serikalini pamoja na ajira mbalimbali zilizotokana na miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa hapa Nchini.

Vijana kwa umoja wao kutoka maeneo mbalimbali nchini wameamua kuchanga hela kwa ajili ya kumchukulia Fomu ya urais mama Samia Mama wa shoka,chuma cha reli, jasiri muongoza njia, shujaa wa Afrika, nuru ya wanyonge,mtetezi wa vijana,simba wa nyika na komandoo wa vita.

Vijana wanafanya haya kuonyesha upendo wao mkubwa kwa Rais samia na namna wanavyomuunga mkono, kumkubali na kuendelea kuhitaji utumishi wake kwa miaka mingine tena. vijana wameguswa na kazi kubwa aliyoifanya Rais samia ndani ya Muda mfupi wa uongozi wake iliyoleta matumaini kwa mamilioni ya vijana.

Hivyo vijana wameona wasikae tu wamebweteka kusubiri kuletewa mgombea ,bali wameamua kuonyesha hisia zao na kupaza sauti zao juu ya uhitaji wao wa kuongozwa na Rais samia kwa muhula mwingine tena. vijana wanataka waweke hatima ya Taifa lao na maisha yao katika mikono Salama ya Rais samia kiongozi msafi, mnyenyekevu, mzalendo, mkalimu, msikivu na mwenye upendo.

Rais samia ndiye chaguo la watanzania, ndiye kiu ya vijana,ndiye aliyeshinda katika mioyo ya vijana.ndio jicho lao lilipotizama kwa matumaini na matarajio makubwa. Hii ndio faida ya kiongozi kugusa maisha ya watu,kuinua maisha ya watu, kuleta matumaini katikati ya kukata Tamaa pamoja na mwanga katikati ya giza.

Lazima watu wakupiganie na wakusemee ni lazima vinywa vyao vilisema na kulitaja jina lako kwa mema,ni lazima watu waziseme sifa zako na kutangaza mema yako. Sasa vijana wanamsemea Rais samia kwa yale makubwa na ya kupendeza aliyoyafanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake yaliyogusa maisha ya mamilioni ya vijana hapa Nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Luca!

Kuna mengi yatajiri hapo mwakani kabla ya huo mwaka was uchaguzi!!

Tuombe uzima,achana na kampenii za kitoto kama hizo!
 
Rais Samia Ndiye Rais wa watanzania mpaka 2030.ndio chaguo la watanzania,ndio kiu ya mamilioni ya watanzania na ndiye anayeungwa mkono na mamilioni ya watanzania na ndiye aliyeshinda katika mioyo ya vijana walio wengi hapa nchini,ambao sasa wameamua kumchukulia Fomu ya Urais uchaguzi ujao ili kuonyesha upendo wao kwake .
Jitahidi walau uwe umepata ajira hata ya mgambo wa jiji kabla bibi yako hajarudi kwao Nungwi.
 
Wapumbavu nyinyi... Tunaojitambua tunataka tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya.

Nyinyi wapumbavu mnategemea armed forces ziendelee kuwaweka IKULU.
Kwani akina mbowe na Lissu walikuwaga wanapita na kutangazwa washindi kupitia Tume ipi?
 
Lucas ndg yangu

Rais Samia Hana kipingamizi kwa maana ni mpango wa Mungu na Chaguo lake.

Uchaguzi wa mwaka ujao kwanzia serikali za mitaa mpaka wa Urais Kila kona ni CCM

Nyumbu wa Ufipani wataweka mpira kwapani soon
Nyumbu mamako msengerema mkubwa wewe
 
Back
Top Bottom