Mkwaruu Kombo-Tapa
Member
- Aug 1, 2020
- 62
- 60
Mku swala la ajira kwa ujumla ninaamini viongozi waliopewa mamlaka kuongoza nchi hii sio creative ya sio wabunifu.Baada ya kufuatilia hotuba nyingi za vyama vya upinzani ninapenda kuwasihi vijana kuwa na tahadhari kwa ahadi zisizoweza kutekelezeka.
Nikianzia suala la ajira ni tatizo la sehemu kubwa duniani watu wamepoteza kazi kwa hali mbaya ya kiuchumi pamoja na tatizo la ugonjwa huu wa COVID19 ulipojitokeza. Suala la kusema kuwa wakishika madaraka wataruhusu wananchi wataruhusiwa kwenda kuishi kwenye hifadhi ni la upotoshaji mkubwa kwani tukiruhusu utekelezaji huo ina maana utalii utakufa.
Ninatoa mfano nchi ya Misri 2011 wananchi walimuondoa madarakani Rais Hussein Mubarak kupitia chama cha Muslim Brotherhood baada ya chama hicho kutoa ahadi nyingi zisizoweza kutekelezeka kufika mwaka 2013 wananchi hao hao waliiingia mitaani kupinga hicho chama matokeo Jeshi la nchi hiyo likatwaa madaraka tena.
Tumeona hapa majirani zetu Kenya baada ya kuiondoa KANU madarakani na kupata katiba mpya leo wakenya wanaikumbuka KANU kwani Ufisadi na ukabila umekuwa mkubwa sana kufikia kuhatarisha umoja wa nchi hiyo. Katika uchaguzi wa mwaka 2007 wananchi kupitia vyama hivyo vilipigana vita vya kikabila na maelfu ya wananchi walipoteza maisha.
Kwa mustakabali wa nchi yetu Tanzania bado CCM ni chama pekee kinachoweza kuipeleka nchi katika uchumi mzuri na umoja wa kitaifa.
Tusijaribu kufanya kosa kubwa la kutoipigia kura CCM na haswa Rais Magufuli ambaye ameleta mageuzi makubwa ndani ya chama hicho na serikali kwa ujumla.
Hivi tuu kwa akili ya kawaida sector ya Kilimo inauwezo wa kuajiri watu wote wasiokuwa na ajira nchi nzima.
Mfano Rais fedha zilizonunulia ndege angeziingiza ktk kilimo cha umwagiliaji leo kiajira tungekuwa wapi. Kingine Watanzania wengi kujiajiri ni kawaida sasa niambie huyu ambaye aliyejiari katika kilimo cha msimu kama Serikali ingemjengea Malambo ya kuhifadhia Maji na kuzijenga Skimu za kupeleka maji mashambani leo hii tusingetumia nguvu kubwa kuomba kura au kulalamika swala ajira. Kwa ujumla chama changu hapa kimechemka kwa huko ktk nchi zingine tumeona serikali zikiondolewa madarakani kwa ajili ya ajira kwa hiyo tangu pale Lowassa alipozungumzia swala la ajira leo hii ni miaka ishirini imepita hakuna ufumbuzi wake. Na pale wasomi wasiokuwa na ajira anavyooji au kuwa na maswali mengi juu ya serikali ya chama changu anaitwa sio mzalendo na kumbuka hawa wanaoitwa sio wazalendo kwa kuuliza yaliyohaki yao wanazidi kuongezeka kila mwaka kwani idadi ya wasomi inazidi kuongezeka kila mwaka na kukosa ajira kwa hiyo tukubaliana na lolote kwani tulipewa miaka mingi ya kulishughulikia hili swala. Na baada wapinzani wetu kujua uwezo wakuongeza ajira wanao ndo maana wamelishikilia kwani strategy .
Hivi inakuwaje Uganda inapitishia mizigo yao ktk bandari yetu then ss watz tunaenda kununua bidhaa kwao badala ya Waganda kuja kununua Tz hivi kweli hii ni akili. Watanzania wa leo sio wajinga kwa wanaona na wanaelewa