Uchaguzi 2020 Vijana kuweni makini kwa ahadi za uongo kutoka Vyama vya Upinzani

Mku swala la ajira kwa ujumla ninaamini viongozi waliopewa mamlaka kuongoza nchi hii sio creative ya sio wabunifu.
Hivi tuu kwa akili ya kawaida sector ya Kilimo inauwezo wa kuajiri watu wote wasiokuwa na ajira nchi nzima.
Mfano Rais fedha zilizonunulia ndege angeziingiza ktk kilimo cha umwagiliaji leo kiajira tungekuwa wapi. Kingine Watanzania wengi kujiajiri ni kawaida sasa niambie huyu ambaye aliyejiari katika kilimo cha msimu kama Serikali ingemjengea Malambo ya kuhifadhia Maji na kuzijenga Skimu za kupeleka maji mashambani leo hii tusingetumia nguvu kubwa kuomba kura au kulalamika swala ajira. Kwa ujumla chama changu hapa kimechemka kwa huko ktk nchi zingine tumeona serikali zikiondolewa madarakani kwa ajili ya ajira kwa hiyo tangu pale Lowassa alipozungumzia swala la ajira leo hii ni miaka ishirini imepita hakuna ufumbuzi wake. Na pale wasomi wasiokuwa na ajira anavyooji au kuwa na maswali mengi juu ya serikali ya chama changu anaitwa sio mzalendo na kumbuka hawa wanaoitwa sio wazalendo kwa kuuliza yaliyohaki yao wanazidi kuongezeka kila mwaka kwani idadi ya wasomi inazidi kuongezeka kila mwaka na kukosa ajira kwa hiyo tukubaliana na lolote kwani tulipewa miaka mingi ya kulishughulikia hili swala. Na baada wapinzani wetu kujua uwezo wakuongeza ajira wanao ndo maana wamelishikilia kwani strategy .
Hivi inakuwaje Uganda inapitishia mizigo yao ktk bandari yetu then ss watz tunaenda kununua bidhaa kwao badala ya Waganda kuja kununua Tz hivi kweli hii ni akili. Watanzania wa leo sio wajinga kwa wanaona na wanaelewa
 
[emoji40][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Awamu ya tano imefanya nini kipya? Reli Tazara walijenga SGR miaka hiyo hivyo sio kitu kipya, umeme wakoloni, Mwalimu walijenga mabwawa mengi tu tunayatumia hadi leo, barabara hizi wakoloni walijenga sio hizi za miaka 3 zimeharibika.

Ccm ndio ina viongozi wahuni, wezi, kwa miaa zaidi ya 60 wamekua wakituibia rasilimali zetu, kutufanya tuwe mafukara na masikini wa kutupwa.

Miaka 60 bado watoto wanasomea kwenye miti kama nyani halafu unatuambia umejenga reli?
 
Naunga mkono hoja.

Huyu mpuuzi Lissu hana atakaloweza kufanya. Hata akichaguliwa japokuwa haiwezekani, atakumbana na upinzani mkali.
 
Mkuu asilimia kubwa ya vijana ni mashabiki wa ahadi zisizoweza kutekelezeka, na hatujiulizi kabla ya kufanya maamuzi ya kubeza hata kile tulichonacho kibindoni, hivi mtu anaposimama na kukwambia nitakupandishia mshahara marambili ya ule wa awali bila ya kuwa na vitega uchumi hiyo pesa ya kukupandisha itatoka wapi?? "Vijana ni viongozi wa taifa la kesho" ni vizuri kutafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi ambayo unaweza kuyajutia mwenyewe.
 
Unamaanisha ahadi za million 50 kila kijiji na laptop kwa kila mwalimu?
 
Je kila kijiji kulipata milioni50 za ahadi ya rais? Je huo si uwongo?
 
yeye mbona anapanda tena ya kukodi ambayo ni gharama kuliko ya kawaida? sema wewe ndie huna hela wenye pesa wanapanda akiwemo Lisu
Eeh Mimi Sina ela kwa sababu ni raia wa chini . Sasa unapojiita rais wa wanyonge hafu unanunua ndege , Je hapa umemsaidia mama muuza mboga, umemsaidia mama mchoma mihogo pale keko magurumbasi. Umetusaidia sisi ambao kila tukienda kupanda daladala tunaomba kwa Mia tatu.

Usipende kuwa shabiki tu, tumia logic .
 
Hoja ya kitoto sana hii kwa mwanza hata asiyesoma aweza kukujibu

Au nenda tu airport Dar kaangalie abiria watoka mwanza wanavyoshuka na samaki wa mwanza
Ndege zimepaisha soko la samaki kanda ya ziwa

Mandege kibao hubeba samaki kwa ajili ya soko la ndani na la nje

Mwanza wavuvi na wauza samaki wanafaidi sana kwa uwepo wa ndege

Pili kodi zinazopatikana kutokana na mauzo ya tiketi ndizo hizo zinaenda somesha watoto wao elimu bure,kutoka mikopo kwa akiba mama na vijana na nk

Pia hizo kodi ndizo zinalipa mishahara ya wafanyakakazi wa serikali ambao hutumia Hiyo mishahara kutunza familia zao na kununua hizo mboga na hiyo mihogo .Kila mtu anunuapo tiketi ya ndege kuna kodi mle inayoenda kumlipa nduguyo aliyeko serikalini ambaye ukiwa hata na harusi hukuchangia kupitia mshahara aliolipwa kutokana na kodi iliyokusanywa kwa waliokata tiketi za ndege!!
 
Kwanini mjinga asiwe mama yako🤔?Yaani umeshindwa kabisa kujaadili kwa hoja,mpaka unaanza kutukana watu?
Mjinga ni wewe, unaetukana wenzako kwaajili ya watu fulani wasiokujua,ambao hata wakishinda,hautapata chochote.Mama yako alikosea Sana kuzaa kima Kama wewe, Ni Bora angezaa hata tofali.🚶
 
Mimi hilo silijui.

Mpeni Miaka mingine mitano azitoe hizo milioni hamsini kila kijiji na zaidi.
Umeshasema hujui alafu unasema apewe tena miaka mitano ili atoe million 50 kila kijiji.

Mataga ubongo mlitoa mkajazwa funza kichwani.
 
Hivi kuna uongo mkubwa zaidi ya ule wa Magufuli aliosema ataigeuza Tanzania kuwa kama ulaya ndani ya miaka mitano tu!

Hivi yule dingi anaijua ulaya kweli?
Serikali hii ambayo hata vyoo vya shule, soko na stendi inaomba kujengewa kwa msaada wa mabeberu au kutembeza bakuli kwa wananchi, itawezaje kuigeza Tanzania kuwa ulaya?
 
Umeshasema hujui alafu unasema apewe tena miaka mitano ili atoe million 50 kila kijiji.

Mataga ubongo mlitoa mkajazwa funza kichwani.
Unazingua mkuu,

matusi hayajengi.

We unadhani huyo Lissu akichaguliwa atatekeleza hizo ahadi zote ndani ya miaka mitano.
 
Kwa akili yako huyo Tundu Lissu na Mbowe wataifanyia nini Tanzania ikiwa wameshindwa kujenga hata ofisi ya makao makuu ya Chadema licha ya kupokea mabilioni ya ruzuku
 
Hujui kitu wewe !! . Hata mifano unayiotoa siyo. Hosni Mubarak hakutoka Muslim brotherhood. Huyo alikuwa dictator kama hawa tulio nao
Na alirithi madaraka baada kifo cha Anuwar Sadat . Kenya hata siku moja hawajawahi kuitamani Kanu !! Wako mbele yetu kwa hatua kubwa sana.

Kama ni ahadi za uongo basi ziko Ccm . Waliahidi Katiba mpya iko wapi ?!, Waliahidi viwanda viko wapi ?!, Waliahidi million 50 kila kijiji, ziko wapi ?! Waliahidi ajira kwa wasomi ziko wapi ?!.

Kuogopa kufanya mabadiliko ni ulemavu tena wa akili. Binaadamu anayeridhika na mazingira yanayomzunguka hata kama ni duni hafai na ndiyo wewe mleta mada.
 
Sasa huyo anayeishi Belgium anaweza kutekeleza ahadi hizo kweli ama anataka atulete matatizo halafu asepee
Ubeligiji alienda kuishi kwa kupenda ?!. Mbona hueleweki ?!. Mlimcharaza risasi kama nyati hamkutaka hata ajitibu ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…