Vijana kuweni makini na UTI Sugu

Vijana kuweni makini na UTI Sugu

Kuna kitu kinaitwa Urethritis nadhani hii shida ndo wengi mnachanganya na UTI kwa wanaume.
 
So Dr I preffer to say that UTI in male is an STD.
Niliumwa UTI, hospitali walinitibu wakiwa na imani kuwa nimepata kupitia ngono, Daktari specialist akawa anawaambia wale madokta wanafunzi kwa kiingereza, "the guy is married, did you expect he would admit to have unprotected sex with an outside partner?" Hiyo ilikuwa ni Mloganzila


UTI ni tofauti na STI. Sijataka kuandika kitaalam sana tutakimbiana.
Tueleze tu kitaalamu dokta, maana hili gonjwa baya sana, linanyong'onyeza mwili mzima, joints nk
 
Asubuhi nimeamka poa, nikawa nimejiandaa kwenda kariakoo, muda ni saa 1:30 asubuhi, ghafla nikahisi maumivu upande wa kulia wa tumbo karibu na kiuno. Maumivu yakawa yanakuja pindi naposimama, ila nikikaa yanapungua. Nikaona nilale (sio usingizi) ili nisikilizie maumivu yaondoke.

Kufika saa 4:30 asubuhi maumivu ndio yakazidi kuongezeka, nikahisi labda nina ngiri, nisije kubasti kende sababu ya msingi wakati hospitali ni karibu tu, nikaelekea Mloganzila. Kwenda kwa Dokta nikajielezea, wapo kama wanne hivi kwenye chumba, Specialist 1 na madokta wanafunzi 3 (wa kike walikuwa 2)..hapo maumivu makali yapo kende ya kulia, wakaniambia nivue boksa nikatii, wakanikagua kagua sana, na dokta akaagiza nikapige ultra sound - nikaenda huko.

Kule ultra sound nako nikakuta wale wataalamu wako 3 pia, nako nikavua boksa na kuanza kupigwa hiyo camera...wakaconfirm kuwa niliyo nayo ni epididymo orchitis, niliporudi kwa daktari kusoma majibu nae akathibitisha hivyo. Hapo maumivu nayopata hayaelezeki, najikaza kiume lakini hali ni balaa.

Nikaulizwa historia ya ugonjwa nikawaeleza kuwa huwa naumwa UTI mara kadhaa na huenda kwenye dispensari na wananipa Flagyl, Amoxylin nk Wakasema hapo sijatibiwa chochote na UTI imekuwa Chronic (sugu).

Jioni hali ikawa mbaya wakanipa kitanda hapo ili wanifuatilie kwa ukaribu, wakaniwekea drip na kunipa dawa ya kumeza inaitwa DOXY, dawa ina nguvu balaa inahitaji ule na unywe maji mengi baada ya kuinywa ama sivyo lazima utapike. Baada ya siku 2 nilipona fresh mpaka leo niko poa. Hiyo ilikuwa mwaka juzi 2021
 
Back
Top Bottom