Vijana mliomaliza vyuo kwanini mnavuta bangi?

Haya mambo yalikuwepo na yataendelea kuwepo. Ni jukumu la kila mmoja kuchukua hatua ya kuona anasaidia vipi vijana kutojiingiza huko. Kabla hatujamlaumu kijana ni vema tukamlaumu Baba Junior na Mama Junior kwa malezi yao ya kishenzi. Nilipokuwa darasa la pili nilijaribu kuvuta sigara tena isiyo halisi ile ya makaratasi nikaonwa na baba. Kipigo nilichopata ni cha maisha yangu yote na sikuwahi kuwaza hata huo ujinga. Siku hizi mama anavaa anavaa kichupi mbele ya mtoto wake wa kiume eti ni vazi la kuogelea.
 
🙌 Kwahiyo shida ni wazazi na sio vijana??
 
Vijana wanapitia wakati mgumu stress za kupoteza muda darasani mwisho ajira hakuna gharama za maisha kupaa uwezo wakusevu pesa haupo wew waache tu vijana waombee tu badala ya kuwalaumu
 
Nafikiri ni upeo mdogo wa kufikiri kuwa "inaondoa mawazo " kumbe sivyo, ni kujiharibu. Nawashauri tu wafanye kazi yoyote ile ili mradi mkono uende kinywani. Kuna graduate nilikutana nae anaendesha bajaji. Vijana acheni kujiangusha, amkeni, ondoa fikra "kuajiriwa" akilini, weka neno "kujiajiri".
 
Vizuri sana mkuu
 
NB
Ushaur wangu Kwa vijana wafanye uhuni Kwa kiwango Cha vumbi (barabara)

Wasifanye uhuni wa kiwango Cha Lami (barabara)

Walio soma Cuba wanaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…