Vijana mnaosoma sheria, jikiteni sasa kwenye sheria za uchaguzi

Vijana mnaosoma sheria, jikiteni sasa kwenye sheria za uchaguzi

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Tanzania inapitia kipindi cha mabadiliko makubwa sana ya kisiasa. Alichojaribu kufanya Magufuli na serikali yake katika hii miaka mitano na resistance aliyoipata hasa kipindi hiki cha uchaguzi ni uthibitisho wa kile ninachokisema. Mfumo wetu wote wa siasa unabadilika mbele ya macho yetu, kuanzia ndani ya vyama, tume ya uchaguzi na taratibu na mifumo yetu ya uchaguzi.

Sina uhakika kama mitaala yetu ya elimu na taaluma yetu ya sheria inaruhusu mtu ku specialize kwenye sheria za uchaguzi (Electoral Laws) kwa mfano. Au labda ni tawi la Constitutional Law. Wajuvi wa mambo watanitaarifu.

Ninachokiona ni kuwa kutakuwa na mahitaji makubwa ya watu wanaoweza kutafsiri vyema na kusimamia maslahi ya kisheria ya wadau mbalimbali katika siasa na hasa chaguzi mbalimbali, ikiwemo vyama vya siasa, wagombea na kwa upande mwingine ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Serikali. Wadau wengine wanaoweza kuwatumia vizuri wataalamu hawa ni vyombo vya habari katika kusimamia maslahi yao na pia hata kutoa tathmini za kisheria katika vyombo hivyo.

Kwa hivyo, kutakuwa na mahitaji ya watu waliobobea katika kuzielewa na kuzitafsiri sheria za uchaguzi na pia watu wenye uwezo wa kuja na mawazo yaliyo bora katika kuboresha sheria, kanuni na taratibu zetu cha uchaguzi.

Changamkieni fursa vijana.
 
Back
Top Bottom