Vijana na Wazee Arusha waahidi kura ya Ndiyo kwa Katiba Inayopendekezwa

Katiba mpya hoyeee........pigia kura ya ndiyo hata kama huijui.sisi tunayoijuwa tunakuwakilisha wewe tuamini usijali.Wazenji sasa mnaweza kopa duniani wa Bara watawadhamini,na msipolipa wa bara watalipa kwa kodi zao.pigia ndiyo haraka saana
 
Katiba mpya hoyeee........pigia kura ya ndiyo hata kama huijui.sisi tunayoijuwa tunakuwakilisha wewe tuamini usijali.Wazenji sasa mnaweza kopa duniani wa Bara watawadhamini,na msipolipa wa bara watalipa kwa kodi zao.pigia ndiyo haraka saana

Pakalolo utaratibu upo na msingi umeainishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa unasema na kusisistiza na kuipa Zanzibar Mamlaka ya kukopa yenyewe kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

261.-(1) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka ya kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake.


(2) Endapo mkopo utahitaji dhamana, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, baada ya kushauriana na kukubaliana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, itatoa dhamana kwa mkopo unaoombwa.

(3) Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 76, Bunge litatunga sheria itakayoweka utaratibu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kudhamini mikopo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Unaandika kutoka Arusha Chini?

Siyo Mbuguni tu, mi natembeleaga hata mitaa ya Mirerani Songambele, kijiweni, Samaksi hata Naisinyai. unataka tukale nyama ya mbuzi ya kuchoma arifu? Usiniache mtu wangu unistue twende wote. Mi nitakuja na nakala ya Katiba Inayopendekezwa ili tunapokula hiyo nyama tukate na shule kuhusu Katiba kwa manufaa ya kuelimishana. Poa mtu wangu pamoja sana.
 

Sasa hapa umefafanua kabla hawajapitisha Jambo.
Walio pigia kura ili ipite walikodiwa mamluki kibao tuliona ilikuwa kazi kweli kweli ila Sababu mpini alishika ccm ikapita.
Yaliyomo sasa yalikuwa wanauwakilishi wa wananchi Sababu ukawa walitoka wakabaki ccm ndani haikutosha hata Yale mawazo yetu tuliyoyatoa kwa tume ya warioba yakatupwa now yakapendekezwa Mapya.
Ila ukishazoea kusema Ndiyoooo hata uambiwaje yaani unakuwa sikio la kufa.
Nchi sasa hivi majanga kila kona sio elimu,sio afya,sio Ajira,sio usafirishaji then huyo huyo anakupeleka Huko ndio anakuambia pokea katiba bora.
Sijui umekula maharage gani wewe hahaha MIMI NIMESHAAMUA KUBURUZWA BASI.
naijeria wamefanya mabadiliko baada ya kuona kilichopo ni takataka why tanzania na tunaanzia katiba mpya.
 
Sio kweli jambo la msingi ni kusimamia maamuzi yako usikubali kuburuzwa kwani tatizo liko wapi ukisema unaiunga mkono Katiba inayopendekezwa?

Mimi siburuzwi kwanini utaratibu na mchakato uvurugwe ndio maana nchi za kiafrika kila kukicha vita.
Juzi bungeni wamepitisha Muswada wa mitandao yaani majanga matupu waliopitisha walikuwa wajumbe wachache yaani nchi hii ni Kero juu ya Kero.
Ila not this time wee kama ushaaidiwa ukuu wa wilaya na team zenu Mie bado najitambua kipi tango mwitu kipi original.Mie kusema NDIYOO NIMECHOKA.
 

Nani kakuburuza wewe au unajiburuza mwenyewe,hayo mawazo yako unayosema yalitupwa unaweza ukanitajia hapa maana unaweza kuongea kitu usichokijua ukadhani unajua,hao unaosema wanauwakilishi wa wananchi walitoka nje ni akina nani?Je ni ninyi mliwatuma kutoka nje?Je kwa kutoka nje walidhani nani atabaki anajadili Maoni yetu,Je una uhakika waliokuwa wamebaki ndani hawakuwa na uwakilishi wa wananchi?

Na kama ni hivyo basi kwa nini leo tunajiandaa kuipigia kura katiba inayopendekezwa?naona una kasoro moja ya kulishwa maneno,unamezeshwa maneno afu unayaleta humu ndani!!!jisimamoe bana!!!!
 
Aliyekutuma mwambie we are not reachable. Kama ni maoni yako toa ya kwako usitusemee sisi wazee kwa ujumla. Kwanza wala ahtujaiona wala kuisoma.

Wewe ni mzembe tu sasa unavyoshadadia umesoma ya nanii unapingapinga tu kama sio mwongo na mnafiki? Afu haufikiki ni wewe peke yako unayeishi kisiwani usiyejielewa unayetamani kila kitu cha nchi hii kiharibike!!! Wewe sio mzee ni kijana unakusanya mawazo ya kijiweni afu unakurupuka sisi wazee kwa ujumla hata aibu huna wewe muongo mkubwa!!!!toka zako nimekushtukia.
 

Mimi nimeshaisoma katiba yote nitapigia HAPANA.
 
Mimi sijapinga wala kukubali kwakuwa sijaisoma. Ila asitusemee kuwa ni wazee wote. Alitukutanisha lini tukaoa hilo tamko? Karibu Tengeru utupe Elimu

si useme tu hujasoma kigugumizi cha nini wewe,kuw muwazi ili utupishe humu tunaojua tuchangie!
 
Mimi nimeshaisoma katiba yote nitapigia HAPANA.

Wewe huniambii kitu kigeugeu mkubwa toka mwanzo unawaza uovu tu afu unajifanya kushawishi watu mtapoteza kura zenu bure sisi ni Ndiyoo, ucpime na mtashangaa katiba mpya lazima ipatikane.
 

Wewe huniambii kitu kigeugeu mkubwa toka mwanzo unawaza uovu tu afu unajifanya kushawishi watu mtapoteza kura zenu bure sisi ni Ndiyoo, ucpime na mtashangaa katiba mpya lazima ipatikane.

Sasa wewe umeona kitu mimi sijaona Jipya bora hata ILIYOPO hakutakuwa na tofauti so wewe kama ni wa Ndiyo na utasema Ndiyo tuu mpk mwisho.
Mimi KUBURUZWA nimeshaacha siku nyingi sana.Mimi ni HAPANA
 
Kamalizeni kuandikisha watu kwanza


Zoezi la kuandikisha watu litafanyika tu maana ndo mpango mzima na kilio cha muda mrefu cha wadau mbalimbali,wanaharakati,UKAWA,wale wasio na vyama ili kutoa fursa ya ingizo jipya kupiga kura hasa waliozaliwa mwaka 1995 ambao mpaka Oktoba 2015 watakua wamefikisha miaka 18. Zoezi hilo litafanyika tu iwe mvua iwe jua maana ndo mpango mzima!ama una hoja nyingine ongea,Katiba mpya ni lazima.
 
Katiba ya Chenge tunaijua, Wazee na Vijana wa Arusha tunawafahamu, NA WEWE NI NANI?


Katiba ya Chenge hatuijui,Wazee na vijana wa Arusha tunawafahamu na tumezaliwa hapa hapa wewe unauliza kwa mamlaka ya nani?Huwezi zuia mafuriko ya mvua kwa ulimi utang'oka meno!!! Katiba Inayopendekezwa haizuiliki!!
 
Sasa wewe umeona kitu mimi sijaona Jipya bora hata ILIYOPO hakutakuwa na tofauti so wewe kama ni wa Ndiyo na utasema Ndiyo tuu mpk mwisho.
Mimi KUBURUZWA nimeshaacha siku nyingi sana.Mimi ni HAPANA

Hujielewi wewe nimekuambia unashabikia mambo usiyoyajua umekata tamaa unaanza kutofautiana na UKAWA wanaotaka Katiba mpya wewe unataka ya zamani ha ha ha ha kweli wewe umetumwa wewe na wala sio Muarusha peleka zako huko!!!
 

UTASHI ZAIDI UNATAKIWA NA SIO USHABIKI.katika katiba tusiangalie hoja yakuwa ni mbaya au nzuri?haiwez kuwa nzur au mbaya jumla lamsingi hoja zinazo zungumziwa kuikwamisha katiba zina maslahi kwa taifa au kundi la wachache? mfano uwajibikaji wakiongoz unamaslah kwa nan? kupunguza nafas za uteuzi badala yake watu wenye sifa waombe kaz lina maslah kwanani? wazir asiwe mbunge ilikutenganisha mihimili ya dola ja kuongeza uwajibikaji na kupanua ajira linamaslah kwa nani?.tuache ushabiki katiba nimaridhiano zipimwe hoja zenye maslah kwa taifa ndizo ziwepo kwenye katiba na sio katiba inayoorodhesha mahitaji ya watu na kuwaacha wachache wayapate yaliyoorodheshwa.
 

Aiseee arife niaje ?? Umedata nini ?? Ni Chuga ipi hiyo chaliii wangu
 

sasa vijana!! hamuwez kuwa sawa kwa kila jambo,kila mtu anamtazamo wake pia mkubali kutokukubaliana.NIVYEMA MTOA MADA USIWEBIASED maana hawawezi kaka kikao wazee 500 na vijana 500 ukasema vijana na wazee wote wamekubali.kwa jiji kama hilo kitafiti sample iliyotumika hainishawishi japo mk nimeweka idadi kubwa lakini bado hainishawishi.KATIBA SIO USHINDANI BALI NIMARIDHIANO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…