Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katiba mpya hoyeee........pigia kura ya ndiyo hata kama huijui.sisi tunayoijuwa tunakuwakilisha wewe tuamini usijali.Wazenji sasa mnaweza kopa duniani wa Bara watawadhamini,na msipolipa wa bara watalipa kwa kodi zao.pigia ndiyo haraka saana
Unaandika kutoka Arusha Chini?
Unaandika kutoka Arusha Chini?
Ndg yangu theki sikubalia nawe kabisa kuwa katiba Imetungwa na ccm nikukumbushe kitu juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Sheria hii Sura ya 83 imezingatia nakusimamia masuala hayo ya Katiba baada ya kuwekwa pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Sheria hii tangu ilipotungwa mwaka 2011 hadi tarehe 31 Desemba, 2013. Hebu soma na jiulize usemi wako upo sahihi juu ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
Kwanza, Uundaji wa Tume Amri ya 2 aya (f), 5. Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, na kwa kuzingatia hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi iliyopo katika Jamhuri ya Muungano, kwa amri itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali, ataunda Tume.
Pili, Uteuzi wa wajumbe wa Tume 6.-(1) Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume. Na Muundo wa Tume hiyo upo kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na.394 la Mwaka 2011 Amri ya 2 aya (h). Kwa hiyo Bunge Maalum liliitishwa kwa Sheria Na. 9 ya mwaka, 2013 Kupitia Tangazo la Serikali Na.394 la mwaka 2011 Amri ya 2 aya (r) ambalo linaundwa na wajumbe wafuatao: (a) wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; (b) wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; (c) wajumbe mia mbili na moja watakaoteuliwa na Rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar kama ifuatavyo: (i) wajumbe ishirini kutoka Taasisi zisizokuwa za Kiserikali;Sheria ya Mabadiliko ya Katiba [Sura ya 83 Toleo la mwaka 2014] (ii) wajumbe ishirini kutoka Taasisi za Kidini; (iii) wajumbe arobaini na mbili kutoka Vyama vyote vya Siasa vyenye usajili wa kudumu; (iv) wajumbe ishirini kutoka Taasisi zaElimu;(v) wajumbe ishirini kutoka katika makundiya watu wenye ulemavu;(vi) wajumbe kumi na tisa kutoka Vyama vyaWafanyakazi;(vii) wajumbe kumi kutoka Vyamavinavyowakilisha Wafugaji;(viii) wajumbe kumi kutoka Vyamavinavyowakilisha Wavuvi;(ix) wajumbe ishirini kutoka Vyama vyaWakulima;(x) wajumbe ishirini kutoka makundimengine yoyote ambayo yana malengoyanayofanana.
Jamani ujasiri wa kusema uongo kiasi hicho unautoa wapi kuwadanganya Watanzania? theki uwe mkweli na mzalendo kwa ukweli wako. Sura hiyo ya Bunge Maalum na wajumbe wake wote ni wa chama kimoja? Ona sasa (iii) wajumbe arobaini na mbili kutoka Vyama vyote vya Siasa vyenye usajili wa kudumu. Acha uongo kama umetumwa kamwambie aliyekutuma Watanzania wamekugundua na hawadanganyiki.
Sio kweli jambo la msingi ni kusimamia maamuzi yako usikubali kuburuzwa kwani tatizo liko wapi ukisema unaiunga mkono Katiba inayopendekezwa?
Sasa hapa umefafanua kabla hawajapitisha Jambo.
Walio pigia kura ili ipite walikodiwa mamluki kibao tuliona ilikuwa kazi kweli kweli ila Sababu mpini alishika ccm ikapita.
Yaliyomo sasa yalikuwa wanauwakilishi wa wananchi Sababu ukawa walitoka wakabaki ccm ndani haikutosha hata Yale mawazo yetu tuliyoyatoa kwa tume ya warioba yakatupwa now yakapendekezwa Mapya.
Ila ukishazoea kusema Ndiyoooo hata uambiwaje yaani unakuwa sikio la kufa.
Nchi sasa hivi majanga kila kona sio elimu,sio afya,sio Ajira,sio usafirishaji then huyo huyo anakupeleka Huko ndio anakuambia pokea katiba bora.
Sijui umekula maharage gani wewe hahaha MIMI NIMESHAAMUA KUBURUZWA BASI.
naijeria wamefanya mabadiliko baada ya kuona kilichopo ni takataka why tanzania na tunaanzia katiba mpya.
Aliyekutuma mwambie we are not reachable. Kama ni maoni yako toa ya kwako usitusemee sisi wazee kwa ujumla. Kwanza wala ahtujaiona wala kuisoma.
Nani kakuburuza wewe au unajiburuza mwenyewe,hayo mawazo yako unayosema yalitupwa unaweza ukanitajia hapa maana unaweza kuongea kitu usichokijua ukadhani unajua,hao unaosema wanauwakilishi wa wananchi walitoka nje ni akina nani?Je ni ninyi mliwatuma kutoka nje?Je kwa kutoka nje walidhani nani atabaki anajadili Maoni yetu,Je una uhakika waliokuwa wamebaki ndani hawakuwa na uwakilishi wa wananchi?
Na kama ni hivyo basi kwa nini leo tunajiandaa kuipigia kura katiba inayopendekezwa?naona una kasoro moja ya kulishwa maneno,unamezeshwa maneno afu unayaleta humu ndani!!!jisimamoe bana!!!!
Mimi sijapinga wala kukubali kwakuwa sijaisoma. Ila asitusemee kuwa ni wazee wote. Alitukutanisha lini tukaoa hilo tamko? Karibu Tengeru utupe Elimu
Mimi nimeshaisoma katiba yote nitapigia HAPANA.
Wewe huniambii kitu kigeugeu mkubwa toka mwanzo unawaza uovu tu afu unajifanya kushawishi watu mtapoteza kura zenu bure sisi ni Ndiyoo, ucpime na mtashangaa katiba mpya lazima ipatikane.
Kamalizeni kuandikisha watu kwanza
Katiba ya Chenge tunaijua, Wazee na Vijana wa Arusha tunawafahamu, NA WEWE NI NANI?
Sasa wewe umeona kitu mimi sijaona Jipya bora hata ILIYOPO hakutakuwa na tofauti so wewe kama ni wa Ndiyo na utasema Ndiyo tuu mpk mwisho.
Mimi KUBURUZWA nimeshaacha siku nyingi sana.Mimi ni HAPANA
Mimi nimeshaisoma katiba yote nitapigia HAPANA.
Vijana wakiwemo na wazee wa Arusha wamevunja mzizi wa fitina kwa kuielewa katiba inayopendekezwa huku wengi wakisema kuwa hawaoni haja ya wao kuipinga na kuichukia katiba hiyo. Kutokana na kuikubali Katiba Inayopendekezwa wanawaomba vijana wenzao kote nchini kuipigia kura ya NDIYO. Huu ni ukweli usiopingika kuwa Katiba hii imejali makundi karibu yote. Nawapongeza wazee na vijana hao kwa hatua waloifikia na naamininTanzania nzima wataamka na kuwa mfano kama hawa. Safi sana.
Vijana wakiwemo na wazee wa Arusha wamevunja mzizi wa fitina kwa kuielewa katiba inayopendekezwa huku wengi wakisema kuwa hawaoni haja ya wao kuipinga na kuichukia katiba hiyo. Kutokana na kuikubali Katiba Inayopendekezwa wanawaomba vijana wenzao kote nchini kuipigia kura ya NDIYO. Huu ni ukweli usiopingika kuwa Katiba hii imejali makundi karibu yote. Nawapongeza wazee na vijana hao kwa hatua waloifikia na naamininTanzania nzima wataamka na kuwa mfano kama hawa. Safi sana.
Kwenye msafara wa mamba na kenge wamo,arusha ni kura ya ndio kwa sisi vijana,hata ww mmoja natumaini si muda mrefu utabadilika tu,najua hujaisoma katiba inayopendekezwa vzr hivyo unatrgemea maneno ya kusikia toka kwa wanasiasa uchwara,akili za kuambiwa changanya na zako,tuko pamoja,karibu kwenye kundi la waliosoma na kuielewa katiba inayopendekezwa,hutajutia,utaelimika vzr na utatoa wingu lililotanda mbele yako. Sema ndio kwa katiba inayopendekezwa