Vijana oeni mabinti wenye kwao

Vijana oeni mabinti wenye kwao

kichomiz

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
19,257
Reaction score
12,244
Habari za juma pili wakuu, wacha leo niwakumbushe kidogo vijanajuu ya kupata wenza wanaokaa makwao.

(1) Usioe binti ambae kwenye familia yao mama ndio Kila kitu. Yaani mama ndio mwenye sauti kuliko baba, akitoa neno tu mpaka baba anaufyata.

Hapo usijaribu kusogeza pua kutaka kuoa, hiyo inakuwa sio nyumba salama bali ni danguro, nyumba yenye heshima huwa na kiongozi anayetambulika na katiba ya Mungu, ukijiingiza hapo jiandae kwa majanga ya copy and paste kutoka kwa mama.

(2) Kuna vijana huwa wanadanganyika binti akitoroka kwao akamfuata geto na kumwambia nakupenda, mimi siwezi ishi bila wewe, nioe na wala sijali nyumbani watasema nini.

Kijana jua hapo hakuna mke, kuna kadada ambako hakana kwao kamekuja kwako kupigwa ukuni tu, mbele ya safari katakusumbua mno. Kama kameshindwa kujali kalipozaliwa na kulelewa, we ni nani kaje kakujali? Hakuna rangi utaacha kuona kakifungua makucha.

(3) Kuna tule ambato tuna pretend, kanajifanya kamtu mbele za watu kumbe ni kafisi hakaachagi hata mifupa. Kastory kidogo kuhusu ka pretend.

Jamaa yangu alikapenda kadada flani hivi akataka kuchumbia. Ukikaona hivi utasema nimepata wife material safi, kabla ya yote kalijifanya kana masharti lundo, hakataki sex mpaka jamaa ajitambulishe kwao, na sisi tukawa wajanja kabla ya kwenda kujitambulisha, tukaona ni bora na sisi tumtambue.

Tukazama kwa wenyeji tukampata SAG akatupa A to Z za huyo mlimbwende. SAG akasema mbona hapo iko nje nje kama ya mbuzi! Duh, tukaona tumfanyie field kuhakikisha kwa kuwa jamaa alikuwa amedhamiria.

Jioni mida ya saa tatu tukasogea maeneo yao, jamaa akamvutia waya mlimbwende akagoma kutoka akidai ni usiku, na mama yake yupo sebuleni. basi jamaa akamwambia nilikuja na bajeti kidogo hapa nilitaka nikuachie.

Alivyosikia bajeti akajua ni hela dakika mbili nyingi akawa amekuja, jamaa akapiga nae story mpaka saa sita ndio karudi ndani, hapo tukawa tumejua hapo hakuna mtu kuna jalala la Kijiji, biashara ikaishia hapo.

Mabinti wenye kwao ni wale waliolelewa katika misingi ya maadili, heshima na utu. Ukianza kuongea nae anakusikiliza vizuri na kwa makini, kisha anakupa jibu stahiki linaloendana na maongezi yako.

Hawakurupuki maana wamefundwa na kufundika, misingi iliyopo kwao na jinsi wanavyoishi kwa heshima, mama anamuheshimu baba na baba anampenda mama, ndivyo alivyo vibeba.

Huyo hawezi kuja geto kwako aseme anakupenda umuoe, kama wale wafata ukuni wasio na makwao, anaiheshimu familia yao na nyumba yao.

Tutaonana baadae.
 
Habari za juma pili wakuu, wacha leo niwakumbushe kidogo vijana
juu ya kupata wenza wanaokaa makwao.

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom