Vijana pendeni nchi yenu, wazungu wamefilisika, hawana cha bure cha kutugawia sisi.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Vijana jengeni nchi yenu wenyewe kwa akili na mikono yenu, wazungu hawana fedha za kutupa tujenge nchi yetu, wenyewe wamefilisika vibaya sana. Hata wazungu wanakwenda China na Uarabuni kuomba misaada ya fedha na wawekezaji waende kwao.

Inawezekana vijana wetu hawajui kuwa wazungu siku hizi hawana fedha, wamefilisika vibaya sana; lakini hebu angalieni namna timu za ulaya (wazungu) zinavyonunuliwa na kumilikiwa na Waarabu, mnadhani zinauzwa kwa waarabu kwa kupenda? Hakuna mzungu mwenye hela za kumudu gharama za kuziendesha. Hebu oneni namna wachezaji wakubwa wa ulaya wanavyokimbilia Uarabuni kucheza mpira, unadhani wanapenda sana kwenda kucheza mpira kwenye joto?

Kuna wahuni wanawabwetesha kwa kuwaambia kama tz ikinyimwa misaada na wazungu tutakufa njaa. Kuna wahuni wanadhani wazungu wana ubavu wa kutulazimisha sisi namna ya kuwapenda, kuwalinda na kuwahudumia watu wetu na mali zao.

Hebu msikilize Professor ambae alikimbia kutoka chama kilee cha chomachoma.

View: https://youtu.be/M9QXLP_-PiY?si=k-NBROoxmie8b5v3
 
Bila shinikizo la kutoka nje CCM mtatuburuza sana
 
Hakunaga fellowship ya usomi na utumwa wa maslahi binafsi. Msomi ambaye ni mtumwa wa maslahi binafsi is worse than a regular fool.

Wahenga walisema, “Usitukane mamba kabla hujavuka mto”! Nchi zinapoamua kukuwekea vikwazo, zitafanya hivyo dynamically (not statically) kuhakikisha objectives za vikwazo zinakuwa achieved. Mataifa ya magharibi (wazee wa fitina) yakiamua kushughulika na jeuri ya Serikali ya mazafakas wa CCM hata nusu mwaka haupiti kabla Watanzania hatujaanza kununua breakfast kwa TZS 5 million!
 

Kuipenda nchi yetu sio ombi. Ni wajibu wetu. Naa kuisaliti nchi ni kosa kubwa kama lile la uhaini au kutaka kuua mfalme halafu ukabainika.

Lakini kwa muda mrefu, upendo wa wananchi kwa nchi yao unavurugwa na tamaa za mali, wizi na ubadhilifu wa mali ya umma, unaofanywa na watu wachache wanaopewa dhamana.

Kiasi kwamba wana kuwa na ukwasi mkubwa, ilhali walio wengi wanachangamoto zisizoeleza za mambo yanayoendana na umaskini.

Nchi yetu kwa sasa ina matabaka....na hilo limeleta mgawanyiko mkubwa wa mitazamo. Kama kweli tunajipenda tuache kudharau wananchi. Tuwajibike kwao jinsi inavyostahili.

Mfano, kule Ngorongoro kuhamisha wale watu kwa mabavu ili aje mwekezaji...mwekezaji gani? Anawekeza nini cha zaidi ya kile ambacho Mwenyezi Mungu alishawekeza? Ukiangalia sana...ni utapeli.

Na hata ubinafsishaji wa mashirika ya umma toka enzi hizo ulijaa mambo mengi yasiyo ya kizalendo na yenye mashaka....

Haya mambo sio madogo...wakubwa na wadogo tushirikiane. Sio wengine wanadaiwa uzalendo na wengine wanatumia dhamana kufanya kila wanachotaka kwa maslahi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…