Matunzo 02
JF-Expert Member
- Jul 7, 2026
- 1,620
- 3,165
Mwanaume unageuzwa ATM daah kuna upendo au tamaa tu?
Mwanaume unageuzwa ATM daah kuna upendo au tamaa tu?
mimi nilikuwa mmoja wao nilikuwa napima uanaume wang kwa pesa mimi binafsi nakushukuru kwa mafunzo yako ndo yakanifanya nijitambue kama kijana huenda nigekuwa mmoja waoNa ukishaingia kwenye mfumo. Ukitoa unajiona bado hujatoa. Unataka kutoa zaidi. Ujue umekwisha
mimi nilikuwa mmoja wao nilikuwa napima uanaume wang kwa pesa mimi binafsi nakushukuru kwa mafunzo yako ndo yakanifanya nijitambue kama kijana huenda nigekuwa mmoja wao
HakikaMungu hahusiki na uchaguzi wako Mkuu.
Kuna mambo hayahitaji maombi.
Ukiweka kanuni zako ukizifuata zinatokea tuu.
Alafu mtu unamchagua baada ya kuona anasifa na anastahili. Sio unampenda ndio unamchagua.
Kinachoanza ni uchaguzi kisha maamuzi, alafu hisia zinakuja baadaye sana huko hata miaka mitatu ishapita
Una akili Sana kakaHao ni matapeli😀😆
Sio kwamba wanajua thamani yako ndio wanataka warudi. Ni kwamba huko walikokwenda wamekwama.
Mtu anajua thamani ya kitu akiwa nacho na sio akikipoteza. Na ataonyesha kukithamini.
Mtu ukiona anaona thamani ya kitu baada ya kitu hicho kuondoka ujue ni kwa sababu amekwama. Mipango yake sio hicho kitu. Ni baada ya kukosa huko alikokwenda.
Ndio maana sisi wengine hatutoagi nafasi ya pili
Mbona sikutani na watHao ni matapeli😀😆
Sio kwamba wanajua thamani yako ndio wanataka warudi. Ni kwamba huko walikokwenda wamekwama.
Mtu anajua thamani ya kitu akiwa nacho na sio akikipoteza. Na ataonyesha kukithamini.
Mtu ukiona anaona thamani ya kitu baada ya kitu hicho kuondoka ujue ni kwa sababu amekwama. Mipango yake sio hicho kitu. Ni baada ya kukosa huko alikokwenda.
Ndio maana sisi wengine hatutoagi nafasi ya pili
Mbona sikutani na watu sahihi jamaniHao ni matapeli😀😆
Sio kwamba wanajua thamani yako ndio wanataka warudi. Ni kwamba huko walikokwenda wamekwama.
Mtu anajua thamani ya kitu akiwa nacho na sio akikipoteza. Na ataonyesha kukithamini.
Mtu ukiona anaona thamani ya kitu baada ya kitu hicho kuondoka ujue ni kwa sababu amekwama. Mipango yake sio hicho kitu. Ni baada ya kukosa huko alikokwenda.
Ndio maana sisi wengine hatutoagi nafasi ya pili
Una akili Sana kaka
Mbona sikutani na wat
Mbona sikutani na watu sahihi jamani
asantePole sana.
Ukiusikiliza moyo wako umekwisha.
Hii Dunia watu wote huutumia moyo wako kama lango la kukunyonya.
Watatu imani, mapenzi na wewe kwa hiyari yako utaona upo sahihi kunyonywa
Hawatataka akili yako itafakari, idadisi, iulize maswali.
Natokaje kwenye Hilo Giza Kaka?Ukiwa gizani huwezi kuona waliojificha. Ukiwa nuruni utaona mbivu na mbichi
Akili yako bado inagiza ndio maana wanaokufuata ni rahisi kukuficha na kujificha usiwaone
Natokaje kwenye Hilo Giza Kaka?
Muda mwingine kumbe unakuwaga na akili umeshusha nuclear kama Oppenheimer
SawqFuraha yako sio wajibu wa mtu mwingine.
Sawq
Mbaga Jr pitia huu uzi.VIJANA, THAMANI YAKO HAIPIMWI NA KIASI CHA PESA ULICHONACHO. USIKUBALI KUINGIZWA KINGI NA WANAWAKE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Vijana wengi leo wanaishi chini ya shinikizo kubwa ili kuthibitisha thamani yao kupitia pesa. Unaambiwa bila pesa huwezi kupendwa, kuheshimiwa au kuwa mwanaume wa maana. Ukiwakuta vijana na ujinga wao kila kitu wanaambiana tafuta Pesa wewe. Na misemo mingine ya kitoto na kijinga jinga.
Hatimaye wengi wao huaanza kutumia zaidi ya uwezo wao ili tu waonekane.
Usikubali kuingizwa kwenye mtego huo.
Unakuta mwanamke mwenyewe sura halina. Umbo hana.
Shule halijaenda.
Hana cha maana zaidi ya makeup na misuko na nywele za katani. Linakuambia huna hela wewe! Tafuta hela wewe.
Alafu kijana unalialia Lia. Unahangaika na kujitesa. Vijana acheni ujinga. Kuweni wanaume.
Ninatumia maneno ya karaha kwa sababu watu wenye dharau, wanaodharau vijana wenzetu hawastahili kuongeleshwa kwa lugha ya heshima.
Najua wapo wanaume ambao wamejaliwa mionekano mizuri, wamebarikiwa pesa, wamebarikiwa kazi nzuri, elimu, vipaji na vyeo. Wao huenda hawajawahi kukutana au kuona wanawake wakidharau wanaume wenzao.
Lakini mimi Mtibeli niliwahi kuona kwa macho yangu. Ninaletewa kesi nyingi sana. Kijana bodaboda anakesha usiku kucha kwaajili ya kumhudumia mwanamke lakini malipo yake ni dharau, kejeli na utapeli.
Nafahamu kuna wanawake Wema. Ingawaje hao ni wachache sana. Tena sana. Hao hawawezi kuumizwa na mambo yasiyowahusu na wao wanajua nazungumzia kitu gani.
Vijana;
Mwanamke anayekupenda kwa dhati hatakupima kwa kiasi cha pesa unachoweza kutumia kwake. Na kama mtu anakuthamini zaidi kwa uwezo wako wa kutoa pesa kuliko utu, tabia, juhudi na mwelekeo wa maisha yako, jiulize kama kweli anakupenda wewe au anapenda kile unachoweza kumpatia.
Hii haimaanishi kuwa usimsaidie mwanamke unayempenda. La hasha. Mwanaume mwenye uwezo na moyo wa kutoa ni jambo jema. Lakini kutoa kwa hiari ni tofauti na kutumia pesa kwa hofu ya kuachwa au kwa kutaka kuthibitisha kwamba wewe ni mwanaume.
Tena wanawake wapuuzi na wale walaghai wanatumia maneno ya vitisho kwamba usipompa mwanamke wako hela atagongwa tuu.
Vijana kugongwa na tabia ya mwanamke mwenyewe. Ni umalaya wake. Ni starehe zake. Haihusiani na wewe kuwa na pesa au kutokuwa na pesa.
Sisi Watibeli moja ya mambo hayatuumizi kichwa ni mwanamke kugongwa kwa sababu tunajua kwa hakika, kwa hakika tutamfukuza bila kusita, kujali matokeo na Bila vikao.
Kisha itakuwa nafasi yetu kuonyesha tunaweza kupata mwanamke mwingine mdogo zaidi, mbichi zaidi, teketeke zaidi. Kiufupi itakuwa kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi.
Usikope pesa ili kumfurahisha mtu. Usitumie mshahara wako wote kwenye starehe kwa sababu unaogopa kuitwa mchoyo. Usivunje mipango yako ya maisha ili tu kumshawishi mtu kwamba unaweza. Au kupewa sifa za kijinga kwamba una roho nzuri. Roho nzuri wakati wanakuchuna ngozi. Roho nzuri wakati wao wanakufanya msukule. Roho nzuri kitu gani. Usiwe mjinga.
Jenga maisha yako kwanza.
Jenga kipato chako. Jenga taaluma na ujuzi wako. Jenga afya yako. Jenga nidhamu. Jenga heshima. Jenga uwezo wa kusimama mwenyewe hata wakati mambo yakiwa magumu.
Usiogope na usiwe na yale mawazo ya kimfumo ya kinyonyaji kuwaza siku ukiwa na shida nani atakusaidia. Hakuna atakayekusaidia wewe. Kwani ulipokuwa na shida nani alikusaidia. Maisha hayahitaji hayo. Roho nzuri sio uwekezaji. Roho nzuri ni wema usiohitaji malipo.
Thamani yako haipo kwenye pochi yako.
Pesa ni chombo; si kipimo cha utu wako. Leo unaweza kuwa na kidogo, kesho ukawa na kingi. Kesho kutwa ukafilisika kabisa. Kinachobaki ni wewe, tabia yako, akili yako, misingi yako na uwezo wako wa kujenga maisha bora na kusimama katika nyakati ngumu za maisha.
Vijana, msikubali kuingia kwenye mashindano ya pesa ili kuthibitisha uanaume wenu. Mwanaume mwenye mwelekeo hajengi maisha kwa ajili ya kuwapendeza watu; anajenga maisha ambayo hata yeye mwenyewe atajivunia.
Usipoteze kesho yako kwa ajili ya kuthibitisha leo kwamba unaweza kutumia. Na wewe unaenda na wakati.
Unapoambiwa wanawake wanaakili, ujue wanaakili kweli hasa kwa watu wajinga na wapenda sifa. Wanaopenda kujitutumua. Vipofu na wenye roho nyepesi.
Mimi nimemaliza. Wale watoa mapovu dawa zenu bado zipo bandarini. Endeleeni kuninyoosha kwa matusi.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Furaha yangu inatokana na mm mwenyewe! Nawezaje kujipa furaha?Ndio code hizo nakupa