Vijana tuendelee kuchukua tahadhari, UKIMWI upo na bado ni hatari

Vijana tuendelee kuchukua tahadhari, UKIMWI upo na bado ni hatari

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Naomba kuwaasa vijana wenzangu tuendelee kuchukua tahadhari, UKIMWI bado upo na ni hatari.

Miezi 4 iliyopita nilifanya ujinga nikalala na mwanamke bila kutumia condom ama bila kumfanyia vipimo vya kiafya kujua hali yake, baada ya ngono tukafanya vipimo na ikagundulika mwenzangu alikua na maambukizi.

Huyo mwanamke nilikua nimefanya nae ngono mara mbili ila kwa time interval ya mwezi mmoja, hii mara ya pili ndio tukafanya vipimo na ikagundulika mwenzangu hakuwa mzima na wakamuanzishia dozi na mimi nikaanza kumeza PEP. Nashukuru baada ya miezi 4 niko salama.

Vijana tuendelee kuchukua tahadhari, Ukimwi ni hatari na unaweza kuzima ndoto zako kwa starehe ya siku ama sekunde chache. Tuendelee kuchukua tahadhari hadi pale chanjo ya Ukimwi itakapopatikana. Nilisikia wakubwa wa Dunia wameazimia kufikia 2030 wawe wametokomeza Ukimwi, ndio unasikia ujio wa chanjo na labda wataleta dawa sio muda mrefu ila for the mean time tuendelee kujilinda.

20210909_171850.jpg
 
Usianze tu kushangilia matokeo kabla ya mchezo kuisha. Bado unatakiwa kupima mara mbili zaidi ndani ya miezi 6 ijayo. Huwezi jua kwenye hivyo vipimo vijavyo majibu yatakuwaje.

Anyway, hongera sana kwa kunusurika na pia kwa kutoa tahadhari kwa vijana wenzako! Kwa bahati mbaya sana, unaweza ukajiapiza leo kutorudia makosa, lakini katika hali ya kushangaza siku nyingine na katika mazingira usiyo yatarajia, unakuta Kamanda unauza mechi tena!!
 
Usianze tu kushangilia matokeo kabla ya mchezo kuisha. Bado unatakiwa kupima mara mbili zaidi ndani ya miezi 6 ijayo. Huwezi jua kwenye hivyo vipimo vijavyo iwapo tu utaufuatavhuu ushauri wangu.

Hongera pia kwa kunusurika na pia kwa kutoa tahadhari kwa vijana wenzako! Kwa bahati mbaya sana, unaweza ukajiapiza leo kutorudia makosa, lakini katika hali ya kushangaza siku nyingine ma katika mazingira usiyo yatarajia, unakuta unauza tena mechi.
Kwa hiyo miezi 6 ijayo ni kwa exposure nyingine sio ile ya mwezi wa 5, ile ndio imeisha hivyo ambayo nilimeza PEP.

Wataalamu wengi wanaofanya kazi kwenye masuala ya HIV na hata WHO guidelines zinataka upime baada ya miezi 3 ama siku 90 baada ya exposure kwa ajili ya kujiridhisha tu ila ukweli ni kwamba unaweza kua certain ndani ya wiki chache inategemeana na kipimo ulichotumia ila hivi vya rapid ndio maximum miezi 3.

Watu wengi wana uelewa hafifu kwamba ukimwi unaonekana baada ya miezi 3, huo ni uongo, ukimwi unaonekana ndani ya siku chache sana baada ya maambukizi inategemeana na aina ya kipimo, ila siku 90 ndio guidelines zilizopo za WHO kama confirmatory tu.
 
Pima tena miezi kadhaa mbele
Ili iweje mkuu?

Guidelines zilizopo zinataka upime baada ya miezi 3 kama tu kujihakikishia kama uko salama ama lah ila kama ni maambukizi unayapata ama yanaonekana ndani ya siku chache sana.

Hakuna kirusi kinaweza kukaa mwilini zaidi ya miezi 3 mwili usi react, hakuna.
 
Hapo kipimo kinamaanisha positive au neg?
 
Ili iweje mkuu?

Guidelines zilizopo zinataka upime baada ya miezi 3 kama tu kujihakikishia kama uko salama ama lah ila kama ni maambukizi unayapata ama yanaonekana ndani ya siku chache sana.

Hakuna kirusi kinaweza kukaa mwilini zaidi ya miezi 3 mwili usi react, hakuna.
Kwa hiyo UKIMWI mtu anapata dalili gani kubwa?
 
Ili iweje mkuu?

Guidelines zilizopo zinataka upime baada ya miezi 3 kama tu kujihakikishia kama uko salama ama lah ila kama ni maambukizi unayapata ama yanaonekana ndani ya siku chache sana.

Hakuna kirusi kinaweza kukaa mwilini zaidi ya miezi 3 mwili usi react, hakuna.
Ndani ya muda gani?
 
Mwezi uliopita nimetimiza mwaka mzima kudinyia ndomu

Nitakuja kuacha nikishajimilikisha jiko
Daah.. ndomu ni kati ya vitu vya hovyo kabisa kuwahi kugunduliwa na wanasayansi. Yani walishindwa kabisa kupata kitu mbadala ambacho labda mtu atapaka, au hata dawa ya kumeza kuzuia maambukizi? Mimi nikimla mwanamke na ndomu wala hua sihesabu kama nilishatembea nae.
 
HATA UPAKAZE MKONGO UKIMWI HAUSIKII MKONGO.
 
Ili iweje mkuu?

Guidelines zilizopo zinataka upime baada ya miezi 3 kama tu kujihakikishia kama uko salama ama lah ila kama ni maambukizi unayapata ama yanaonekana ndani ya siku chache sana.

Hakuna kirusi kinaweza kukaa mwilini zaidi ya miezi 3 mwili usi react, hakuna.
mkuu upo sahihi! hakuna kirus kinakaa ndani ya mwili miezi 3 mwili usipate reaction yoyote nasema hakuna!! Broo nina story hapa ya kwako ni afadhali mara 1000 nitakuja kushuka uzi hapa siku nikikaa poa!! Mimi Mungu kaninusuru tu nimeponea kwenye Tundu la sindano!!! Ahimidiwe Mungu mwenye enzi yote!!

Nina story nzito kidogo!! Ilaa sasa nina miezi 5 naendelea vizur!
Hiyo reaction ya virus ndani ya hiyo miezi 3 inakua sio ya mchezo mchezo..lazima utajua tu hapa hakuna usalama!! Mungu azidi kutunusuru na kutowanyooshea vidole wengine sababu hakuna ajuae kesho yake!! Vijana wengi wanapita sehem hatari
 
Daah.. ndomu ni kati ya vitu vya hovyo kabisa kuwahi kugunduliwa na wanasayansi. Yani walishindwa kabisa kupata kitu mbadala ambacho labda mtu atapaka, au hata dawa ya kumeza kuzuia maambukizi? Mimi nikimla mwanamke na ndomu wala hua sihesabu kama nilishatembea nae.
nimecheka sana kwa kweli..,,ni kama umesema kweli vile

hahahhahah mbavu zangu
 
Mwaka jana mwezi wa 10 nilichapa mwanamke mmoja hiviwa mtaani, baadae nikaja kushituka nilivyoona analiwa na jamaa yangu mmoja hivi ambaye ameathirika zamani sana (miaka ya 2006).

Nilipofatilia nikaambiwa kuwa hata huyo mwanamke ni muathirika kitambo tu, aiseeeh nilikosa amani kwa zaidi ya wiki moja na baadae nikaamua kuwa sitakwenda kupima mpaka pale nitakapozidiwa kwa ugonjwa wowote ule.

Sasa ni mwezi wa 9, na imepita 11 tangu nifanye nae mapenzi bila kuugua chochote najua sina UKIMWI, ila kuanzia siku hiyo nimekuwa mtu makini sana kwenye maswala ya mapenzi.

UKIMWI UPO NA UNAUA, tena sikuizi nadhani Kati ya watu kumi mmoja anakuwa nao.
 
Yaani wewe kama Mimi huwa najipa miezi,nikiona Niko poa najua niko sawa
 
Back
Top Bottom