Kuna watu wa aina nne tu ya wadau ili mchezo wa weka pesa na mwingine aweke pesa halafu mmoja apoteze mwingine apate lifanikiwe.
Kuna Investor: Anachopata ni ROI
Kuna Broker : Anachopata ni Commission
Kuna Tapeli/Anayetapeliwa: Wewe upo kundi hili, Hawa kazi yao ni kunyang'anyana fedha zao na wakati wanafanya hayo wanawagawia hao wawili hapo juu na serikali sehemu ya fedha.
Serikali: Anachopata ni kodi.
Siku zote usifanye biashara ambayo hakuna mambo haya:
Pesa vs bidhaa, Mfano Tsh 500 vs Mswaki
Pesa vs huduma, Mfano Tsh 500 vs matibabu
Bidhaa vs bidhaa, Mfano Maembe vs Sukari
Huduma vs huduma, kulima shamba vs Matibabu.
Ukiona biashara ya weka pesa vs mwingine aweke pesa halafu mmoja apoteze upate wewe nyingi jua hufanyi biashara, unatapeliwa au unatapeli mwingine ambapo aliyetapeliwa anamgawia aliyemtapeli pesa, aliyetapeli anamgawia aliyewekeza, serikali na broker sehemu ya fedha aliyotapeli.
UAMUZI NI WAKO.