Vijana tujifunze kuwa waaminifu. Angalia jinsi Dola 100 ilivyotaka kunitoa roho

Vijana tujifunze kuwa waaminifu. Angalia jinsi Dola 100 ilivyotaka kunitoa roho

Nlipoteza urafiki na bro mmoja hivi alikua ananipa deals za hapa na pale kwa tamaa za betting nika stake hela yake alf mkeka uka chanika, aisee sita sahau
😁😁😁 Mimi Hela ya mtu ninaiogopa sana nyinyi mnawezaje !?
 
Bila kupoteza muda niende direct kwenye Mada mwaka jana ulikuwa mwaka wa changamoto sana kwenye maisha yangu hii yote ni kwa sababu ya kukosa uaminifu kwenye mambo madogo madogo.

Kuna bro ni rafiki yangu lakini kwa sasa ni kama ndugu yangu tupo kwenye urafiki zaidi ya miaka kumi tulisha saidiana vitu vingi siwezi vyote vitaja hapa kuanzia biashara familia matatizo tofauti tofauti amekuwa akinisaidia kama ndugu yake. Namaliza chuo mwaka mmoja mtaani akanifanyia connection alipokuwa anafanya kazi.

Vitu vingi amekuwa akinisaidia kama ndugu yake sasa mwaka juzi alipataga mchongo akaenda uturuki kufanya kazi kwa hiyo tukawa tu tunawasiliana nae kwa njia ya simu.
Sasa kipindi cha nyuma tulikuwa tukijihusisha na hizi mambo za forex nadhani wengi mtakuwa mnaelewa ilishaongelewa sana humu na yule tapeli Ontario.
But niliachaga kufanya hayo mambo kutokana na kupata hasara zisizoisha. Lakini huyu jamaa yangu alikuwa bado king'ang'anizi sasa baada ya kufika huko turkey akawa anashindwa kufanya hizo forex kwa sababu account yake ilikuwa nikama imefungwa hapo ndio shida ilipoanzia.

Kwa sababu mimi nipo huku bongo na account ninayo na alikuwa ananiamini 100% ikabidi aniombe awe anafanya hizo mambo kwenye account yangu yaani ananitumia pesa na weka kwenye account yangu kisha namtumia password na log in kule yeye anaendelea kufanya biashara.

Sasa akawa ananitumia pesa kwa mwezi hata mara mbili anaweza tuma dola 100 au 150 au 50 but kila nikimuwekea anaishia kupoteza zote .But nikaja kufikiria nikaona mbona kibongo bongo jamaa anapoteza pesa nyingi nikapata wazo ngoja nifungue Cent account alafu nimtumie awe anafanyia hizo forex huko.

Kwa ambao hamjui cent account ni account ambayo ukiweka mfano dola 1 kwenye account inasoma 100 ukiwekq 2 inasoma 200 yaani inaongeza sifuri mbili mbele hii yote nikwamba jamaa akinitumia mfano dola 100 naweka dola 1 tu but kule kwake inasoma 100 halafu hizo pesa anazo poteza kwa broker nitakuwa nachukua mimi.
Nilifanikwa kufanya hivyo kama mara mbili tu mara ya tatu akatuma dola 100 mimi kama kawaida nikaweka mfukoni dola 99 nikamuwekea dola 1 yeye anajua kuwa anatrade dola 100 kumbe ni Cent account ikapita kama wiki Mbili najua lazima atapoteza daa kwenda kucheki nakuta kapandisha hadi dola 1200 hapo yeye anajua ana dola 1200 kumbe ni Cent kiuhalisia ni dola 12 ndio zipo.
Daa kijasho kikaanza kunipanda nasema akianza kudai hiyo pesa nitatoa wapi.

Sasa siku nilipopata ugonjwa wa moyo nimetoa Dar nimefika entebe Airport nasubiri gari niende Kambala nikaona simu yake watsup akanambia joohs huwezi amini unajua nimepandisha ile account imefika shingapi wewe jaribu kuotea nikasema sijui akasema chungulia uone daa kwenda kuangalia nakuta imefika dala 6800 kudadadeki nilitamani nidondoke chini milioni karibia kumi na nne halafu kiuhaliasia ni dola 68 tu ndio zipo nitatoa wapi hiyo pesa na sina hata milioni 1 kwenye saving.

Balaa likaja nyumbani kwao wakilia shida tu kidogo ananiambia toa dola 100 mtumie mama hapo nawewe kama unashida toa hata 20 utumie inabidi niingie mfukoni mwangu nitoe hiyo pesa nitume yaani nilihisi kuchanganyikiwa.

Nikaacha kufanya kazi zangu muda wote nikawa naangalia ile account kuna siku nikakuta amenunua gold inapanda ikawa inakimbilia dola 10,000 nikasema hapa sasa ndio kuzima simu na kutokomea .
Yaani siku ile sijui nini kilitokea usiku kama wa saa nne nakuta Gold imeshuka thamani gafla jamaa profit zote zimegeuka loss. Nikawa naomba mungu akaunti yote iteketee maana pesa ya kulipa nilikuwa sina kesho yake by saa 6 mchana Gold ilishuka kama mshale Account yote ikaungua.

Jamaa alinipigia simu ana huzuni kuwa pesa zote zimeteketea kisa tamaa hakujua ile siku nilikuwa nafuraha mno nilihisi nimetua mzigo deni la milioni 20 ningetoa wapi hiyo pesa kimzaa mzaa .

Nilijifunza umuhimu wa uaminifu hata kwenye vitu vidogo vidogo.
Chai
 
Back
Top Bottom