plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,394
- 1,434
Ulimwengu wa sasa umebadilika tofauti na miaka ya nyuma na njia za kujiingizia kipato kwa nyakati hizi ni tofauti na kipindi cha nyuma. Zamani mtu unaweza kuamka huna hata shilingi kumi na ukatoka mtaani ukapata chochote na usilale njaa, lakini kwa nyakati hizi ukiwa katika hali hiyo unaweza ukajikuta siku nzima umeambulia patupu.
Vilevile kwa nyakati hizi ni rahisi ni rahisi sana kumiliki utajiri mkubwa tofauti na hapo miaka ya nyuma. Ukijaribu kuchunguza mtandaoni sasa hivi hapo utakuta kuna vijano wadogo kabisa wa miaka 18, 19, na 20+ wanamiliki utajiri mkubwa wa kuanzia dollar za kimarekani milioni moja na kuendelea, na wengine wachache wa umri huohuo mdogo wanamiliki utajiri wa dollar za kimarekani billion moja na kuendelea, kitu ambacho ni ngumu sana kwa miaka ya nyuma kukuta rundo la vijana wadogo namna hiyo kumiliki utajiri mkubwa kiasi hicho.
Lakini pamoja na baadhi ya watu kwa nyakati hizi kumiliki uchumi mkubwa namna hiyo, bado asilimia kubwa ya watu duniani ni maskini na wanapitia maisha magumu. Kwa nchi zinazoendelea kama hivi pia vijana wengi licha ya kuwa baadhi yao wana elimu ya chuo kikuu, bado wengi wao wanapitia ugumu wa maisha kutokana na ajira kutokutosheleza wingi wa watu katika nchi hizi.
Kutokana na mabadiliko haya na hali iliyopo sasa nawahasa vijana wenzangu tujiingize kwenye shuhuli mbalimbali zitakazoweza kututengenezea pesa kupitia mitandao ya intanenti ili kuweza kujikwamua sisi binafsi kutoka kwenye umaskini na pia tuweze kuinua uchumi wa nchi zetu hizi zinazoendelea, kwani tukianza kupokea mapato tutalipa kodi na kuanzisha shughuli zingine za kiuchumi ambazo nazo zitakuwa zimezalisha ajira kwa wengine na kuinua maisha ya wengine na taifa kwa ujumla.
"Crypto currency" ni moja ya njia ambazo ukijiingisha na kutilia nia inaweza kubadilisha maisha yako kwa baadae, hii ni kwa sababu kunakuwa na idadi flani ya coin(sarafu) ambazo haziongezeke, zinakuwa mined(kuvunwa) na kisha kuwa releazed(kuachiliwa) ili zitumike kama mbadala wa fedha kufanya manunuzi mbalimbali, kubadilisha kuwa fedha, kubadilishana fedha na sarafu kwa kununua idadi kadhaa ya sarafu kutoka kwa mtu mwingine n.k n.k
Sarafu hizi zipo nyingi kwa sasa kama Bitcoin, Pi na wenzake wengi hivyo ni wewe tu kuchagua ujiingize wapi. Uzuri wa sarafu hizi huwa zina idadi maalumu hivyo ni ngumu sana kupoteza thamani yake(kama tunavyojua kitu kikiwa adimu au kwa uchache kinakuwa na thamani kubwa) tofauti na fedha kwani kilasiku matrillion ya fedha mbalimbali duniani yanazalishwa(printed) kitu ambacho kinafanya thamani ya fedha kushuka na ndiyo maana si ajabu kukuta thamani ya Bitcoin moja inapanda kila kukicha, ni kwa sababu fedha zinazalishwa kila siku kiasi cha kupoteza uadimu wake. Hivyo badala ya kuridhika na kubadilishana muda wako na kiwango flani cha fedha(fixed income), kwa walioajiriwa, huku thamani ya fedha ikizidi kushuka kila kukicha, jaribu kutizama sarafu hizi kwa jicho la tatu, kisha fanya chaguo sahihi na uenda miaka kadhaa mbele ukapata uhuru wako kiuchumi.
"Forex Trading", biashara ya kununua fedha ishukapo thamani na kuiuza inapopanda thamani inayofanyika mtandaoni, ambayo soko lake kwa siku linazungusha zaidi ya dollar za kimarekani trillion 6, ni biashara ambayo ukijiingiza unaweza ukajikwamua na kuondokana na umaskini, biashara hii inahitaji uwe na ufahamu wa kulielewa soko na tarajia faida na hasara. Biashara yeyote ile duniani usipokubaliana na uwepo wa faida na hasara wewe bado hujaiva kuwa mfanya biashara.
YouTube na TikTok na mitandao mingineyo kama hii inaweza pia kukuinua kiwango flani kwenye maisha, unakuwa unalipwa kutokana na matangazo, idadi ya watazamaji na bei inatofautiana kutegemeana na watazamaji wako wanatokea nchi gani, kwa mfano nchi zenye uchumi mkubwa kama Marekani, Australia, Russia na wengineo zina CPM(Click Per Mile) kubwa kutokana na uwezekano mkubwa wa kununua bidhaa au huduma zilizotangazwa kwenye matangazo yaliyopitishwa kwenye video yako tofauti na nchi zenye uchumi mdogo.
Vilevile unaweza ukalipwa na Sponsors(haya ni makampuni au watu ambao unaingia nao ubia utangaze bidhaa yao au huduma yao kwenye video yako na wakulipe kiasi gani), pia kwa kupitia Affiliate marketing ambapo baada ya kutangaza bidhaa au huduma ya mtu utaweka link kwenye maelezo ya video yako(description) na utapata asilimia kadhaa kwa kila mauzo.
Kinachohitajika hapa ni kutafuta mada ambazo zitakujengea wafuasi ili uweze kufikia kiwango ambacho unaweza kuanza kupokea mapato, mada zinazozungumzia fedha na uchumi zina CPM kubwa, hii ni kutokana na watazamaji wa mada hizo, wengi wana uwezekano mkubwa wa kununua bidhaa au huduma ambazo zinapitishwa kwenye matangazo.
Njia zingine ni kuanzisha shule za mitandaoni, ambazo utakuwa unafundisha jambo ambalo unalifahamu kwa kina na ukapokea ada kila mwezi. Pia unaweza ukatengeneza website mbalimbali ukaziuza au aplikesheni mbalimbali na ukaziuza au ukazitumia mwenyewe.
Nyingine ni kupitia kufanya kazi mbalimbali za Fleelancing na utakapomaliza kazi ya mtu akakulipa kiwango mlichokubaliana.
HITIMISHO
Kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia na njia ya kuingiza kipato zimebadilika ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Ambapo kwa sasa uwepo wa mashine mbalimbali na maroboti umechukua nafasi ya binadamu na kusababisha ukosefu wa ajira hasa kwa vijana wengi. Tumaini la pekee pamoja na njia zingine zilizobakia ni kujiingiza kwenye shughuli za mitandao ili kujikwamua sisi binafsi pamoja na kuinua nchi yetu.

Upvote
7