Vijana tumechoka ahadi, tunataka matokeo, Sio maonyesho!

Vijana tumechoka ahadi, tunataka matokeo, Sio maonyesho!

2. Mikopo ya Vijana – Masharti Yanaua Ndoto
Kuna kelele nyingi kuhusu mikopo ya vijana, lakini uhalisia wake ni tofauti. Masharti ni magumu kiasi kwamba vijana wengi wanashindwa kufikia. Kama kweli mnataka vijana wajiajiri, basi wapeni mitaji kwa kuzingatia uwezo wao na ubunifu wao, si karatasi pekee.
Good point
 
4. Fursa za Nchi Jirani – Fungulieni Vijana Milango
Kuna fursa nyingi nje ya mipaka yetu. Serikali iweke mazingira ya kuwawezesha vijana kwenda kufanya biashara kwenye nchi jirani kwa urahisi, huku mkihakikisha mapato yanarudi nchini. Hii itasaidia kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza mzunguko wa pesa.
Very Good Point
 
5. Hatutaki Show Off—Tunataka Matokeo
Hatutaki tena kuona ziara, picha na matangazo ya kuonesha kama kazi inafanyika. Mpiga kura wa leo si wa zamani—anataka matokeo ya vitendo, si maonyesho. Badilikeni. Fanyeni kazi zionekane kwenye maisha halisi ya wananchi, si kwenye kamera pekee.
Yeah yeah yeah, another good point
 
Vijana hatuombi huruma—tunaomba haki, fursa, na mifumo inayofanya kazi. Tukipewa mazingira sahihi, tuna uwezo wa kubadilisha taifa hili.

Tumechoka na drama. Tunataka matokeo. Sasa.
Hili ni moja ya bandiko bora nililosoma siku ya leo, nimetoka kujadili haya masuala na mtu wangu mmoja hapa naingia humu nakuta hayahaya tuliyokua tunajadili yameandikwa humu au ulikua unachukua notes mkuu?
 
Kwa hiyo kwa akili yako ,unategemea vijana wote wawe na maisha mazuri😅😅

Dunia hii ya sasa, hamna kitu kama hicho...Tafute kazi tu ,huko vijijini hamtaki kurudi mkishafika Dar..Mkome na mrudi kwenu.
 
Bado hamjasema! Na mtasema tu... kuna vitu vingi vinahusu vijana vifanyiwe reforms. Waziri wa vijana anatembea na kamera anapiga picha anaendesha baskeli, anaaminisha wtanzania kuwa "Umaskini ni uzalendo"
 
Back
Top Bottom