Kijana ukiwa na uwezo mzuri wa kufanya vitu kwa namna yoyote ile, pambana kisha ukishatusua rudi kwa hawa vijana wengine wavivu wa kufikiria na kufanya wape hamasa kisha wakupe hela. Tena wachaji pesa kubwa zaidi akili ziwakae Sawa mpaka watakaposhtuka.
Vijana wa hili taifa ni wajinga sana... Mtu anashinda kufanya betting then anakuja kuandika Sirjeff mwizi...
Huyu jamaa sijuani naye ila ukweli ni kwamba the guy is a real Hustler na siyo mshikiwa akili na wanasiasa kama vijana wengi walivyo.
Kijana unayejielewa tumia kundi lisilojielewa wakiunue zaidi.
Fursa zipo ndugu zangu great thinkers.
Hawa vijana muda wa kufuatilia mambo ya msingi hawana, wao ngono, michezo ya bahati nasibu na kuigiza maisha ndiyo kipao mbele huku wakitamani utajiri wa haraka.
Ngoja tuendelee kusuka mitego, nyie endeleeni kuilaumu serikali na kutukana waliotoboa kabla yenu mkiamini ni matapeli ilihali uvivu wa kufikiri ndiyo tatizo mpaka ukaibiwa.