Vijana wa 2000 watasema hii ni pakiti ya majani ya chai🤣

Vijana wa 2000 watasema hii ni pakiti ya majani ya chai🤣

Mwaka 2001 Nilikuwa na Demu wangu sijui kama anatumia hiyo kitu.. Sasa msimu wa likizo kuna siku nikaenda kwao.. Nikashinda naye.. Kumbe alikuwa na alosto akawa hataki nijue anatumia Kuber.. Akawa kakausha.

Basi mimi sijui nikaaga nikasepa kama dk tano nikagundua nimesahau simu yangu kuifuata nakuta demu mdomo mzito. Nikamuliza vipi tena Asee akani onesha pakti akanambia anabwia..

Basi Nakumbuka kesho yake nili msindikiza mgeni apande treni.. Pale stesheni Si nika uona Nakumbuka ulikuwa unauzwa Jero nika nunua, nikaifungua ile harufu yake kama karafuu nika ichukulia powa.. Nika ibwia kama yote.. Thubutuuu.....

Sitasahu hiyo siku.. Nilitokwa Jasho nilijamba.. Nili nyong'onyea, Mwili ukakosa nguvu.. Ilibidi nika harishe.. Kwanza.. Baada ya hapo Nilikuwa nikiiyona hiyo pakti natapika..
We utakuwa ulimeza ww hatari sana hii kitu nakumbuka sekondari nipo from 2 Kuna best yangu alibwia hyo Alafu tulikuwa na paper la taifa Yani tunaingia kwenye room yeye baada ya kupewa mtihani akalalia meza mpaka msimamizi akaja kumshtua ni Bora tu walivyozipiga marufuku
 
Kulikuwa kuna hii kuber halafu kuna nyingine inaitwa ZIM... Ah balaa sana..

Huwa nacheka sana nikikumbuka mambo ya zamani halafu Nikilinganisha na hawa Gen Z ndio nacheka zaidi
 
Kuber haikuwa ya kunywa yalikuwa majani majani makavu unabwia tu kama tumbaku, ujuchanganye sasa umeze! Wenye kuharisha waliharisha, kushindwa kunyenyuka, unasweat kama una TB😀😀😀 ila haikuwa rafiki ukiila una njaa
Ilikuwa inawekwa chini ya lips ni mwendo wa kutema mate kama nyoka
 
Back
Top Bottom