Vijana wa 2000 watasema hii ni pakiti ya majani ya chai🤣

Vijana wa 2000 watasema hii ni pakiti ya majani ya chai🤣

Ilipigisha sana Suspension "machek Bob" enzi zake inafichwa kwenye mabomba/square pipes ya miguu ya viti.

Nashukuru sikuwahi kuwa mtu wa mikumbo enzi za utineja.
 
Hii ndio ingewaondoa CCM madarakani, walisanuka mapema. Vijana, wazee mpaka watoto walikuwa wanaenda kudata mazima.

Stimu za huyu mhindi zimewahi nilaza makaburini nikijua nipo maghetoni kwenye banco kumbe nimelala juu ya mafuvu kibao.
 
Mwaka 2001 Nilikuwa na Demu wangu sijui kama anatumia hiyo kitu.. Sasa msimu wa likizo kuna siku nikaenda kwao.. Nikashinda naye.. Kumbe alikuwa na alosto akawa hataki nijue anatumia Kuber.. Akawa kakausha.

Basi mimi sijui nikaaga nikasepa kama dk tano nikagundua nimesahau simu yangu kuifuata nakuta demu mdomo mzito. Nikamuliza vipi tena Asee akani onesha pakti akanambia anabwia..

Basi Nakumbuka kesho yake nili msindikiza mgeni apande treni.. Pale stesheni Si nika uona Nakumbuka ulikuwa unauzwa Jero nika nunua, nikaifungua ile harufu yake kama karafuu nika ichukulia powa.. Nika ibwia kama yote.. Thubutuuu.....

Sitasahu hiyo siku.. Nilitokwa Jasho nilijamba.. Nili nyong'onyea, Mwili ukakosa nguvu.. Ilibidi nika harishe.. Kwanza.. Baada ya hapo Nilikuwa nikiiyona hiyo pakti natapika..
Kube for Better Health of your Child😂😂
 
2001 hukuwa na umri was kujielewa.Umefurahisha kijiwe tu. Et umesahau simu nyumbani kwa demu wako 🤣🤣 wakati huo simu sio kitu cha kila mtu anayo. Then unasema 500 kuber!!! Unaijua mia 5 ya mwaka 2000?? Kumbuka mtoto wa kishuaa ndio anaenda shule na 50. Hapo ananunua embe la kukata sh 10 au zima sh 30. İnaweza kupata maji ya kifuko sh 5, ubuyu sh 5,muhogo sh 5. Tumenunua sana Kuber kwa hela za shule haikufika jero. Bia yenyewe haikuuzwa jero mwaka 2000
2000 hapo soda ilikua sh 100. Bia ilikua zaidi ila nafikiri jero ilifika
 
me nilikuwa nanunua mkanda mzima zilikuwa kama 20 ivi naenda nazo shule (boarding) fizi ziliungua zilibadilika zilikuwa nyeusii wakati nipo likizo home niaharudi chumba kilikutwa kimejaa makiberi tupu niligombezwa sana!
Inaonesha ulifanana na Chai Jaba Family 😂😂😂😂Meno Uketo au maindi choma
 
View attachment 3315466

Hii kitu ni bora ilipigwa marufuku maana ilikuwa imeshaanza kula vijana hadi watoto wa primary☠️
Daa kitambo sana....Nakumbuka Tupo Tunasoma mafundisho ya kipaimara 2004 iyo kuna mwamba akaja nayo church...Mara paap Mchungaj kazama class kanikuta nimeishika asee alinipa Kipigo na haikutosha akaenda kunisemea kwa Bi mkubwa kuwa navuta kuber.
Bi mkubwa kidogo aniue
 
View attachment 3315466

Hii kitu ni bora ilipigwa marufuku maana ilikuwa imeshaanza kula vijana hadi watoto wa primary☠️
Nakumbuka siku nimekula kuberi nilishindwa kuvuka barabara, na maza alikuwa amenituma. Story imeanza nmepewa maelezo ujumbe natakiwa niufikishe mahali, sasa baada yakupata hayo maelezo kama ilivyo ada mtoto hanaga safari moja lazima apitie mahali ndio aelekeee mahali anaenda

Katika kutembea mara nmekutana na marafiki wana kuberi, basi nikajaribu bahati yangu, weka kuberi mdomoni kama ugoro unavyoweka, baada ya dakika 3 kitu kikaanza ku kick in mzee, saa hiyo nikiwa natembea naelekea nilipotumwa, ikafika mahali nikashindwa kutembea.

Ikabidi nikae chini bahati nzuri akapita jirani akaniona nmekaa pembezoni mwa barabara ya lami akawa anaongea na mimi nashindwa mjibu ndio akanibeba mpaka home.

Kufika home nashindwa kuongea sababu ya kuberi kuchek mdomoni maza kakuta kuberi! Aiseee nilikuwa kichapo lakini sikusikia chochote maana muda huo niko kwenye ganzi.

Ganzi kuja kuisha aisee mwili wote ni maumivu kipigo cha maza. Mungu alivyo mkubwa ikaja kupigwa marufuku maana wahindi sio watu wazuri
 
Daaah nimekumbuka mbali sana ,....mwanangu mmoja hiv ilikuwa inauzwa sh 300 ....nilikuwa kuiacha baada ya kupigwa marufuku
 
Back
Top Bottom