Vijana wa 2000 watasema hii ni pakiti ya majani ya chai🤣

Vijana wa 2000 watasema hii ni pakiti ya majani ya chai🤣

Mwaka 2001 Nilikuwa na Demu wangu sijui kama anatumia hiyo kitu.. Sasa msimu wa likizo kuna siku nikaenda kwao.. Nikashinda naye.. Kumbe alikuwa na alosto akawa hataki nijue anatumia Kuber.. Akawa kakausha.

Basi mimi sijui nikaaga nikasepa kama dk tano nikagundua nimesahau simu yangu kuifuata nakuta demu mdomo mzito. Nikamuliza vipi tena Asee akani onesha pakti akanambia anabwia..

Basi Nakumbuka kesho yake nili msindikiza mgeni apande treni.. Pale stesheni Si nika uona Nakumbuka ulikuwa unauzwa Jero nika nunua, nikaifungua ile harufu yake kama karafuu nika ichukulia powa.. Nika ibwia kama yote.. Thubutuuu.....

Sitasahu hiyo siku.. Nilitokwa Jasho nilijamba.. Nili nyong'onyea, Mwili ukakosa nguvu.. Ilibidi nika harishe.. Kwanza.. Baada ya hapo Nilikuwa nikiiyona hiyo pakti natapika..
Demu Bado upo nae.?
 
Kuber hiyo sijui iliuzwa 300 akati inatoka na viroba vya Zed vikinukia flavor ya pineapple nlitoroka sana shule kuvitafuta akiiii nlikuwa sifai
me nilikuwa nanunua mkanda mzima zilikuwa kama 20 ivi naenda nazo shule (boarding) fizi ziliungua zilibadilika zilikuwa nyeusii wakati nipo likizo home niaharudi chumba kilikutwa kimejaa makiberi tupu niligombezwa sana!
 
Acheni tuu wakuu namlaumu Binamu kunifundisha ila namshukuru kunifundisha kwa kiasi.

Pia Mungu Amrehemu Alikeshi wa Arusha kwa kuileta Kuber Arusha kwa kuwa alijinyonga baadae.

Kuberi Ilikuwa Hatari Sana.
Kww nini alijinyonga mkuu, ilimuharibu kichwa,!?
 
Kuber ukiwa na kichwa mbovu ukiieka mdomoni ukiwa umekaa chini kwa mara ya kwanza hunyenyuki, ukiweza unaweza tembea umeinama ukihofia kugonga nyaya za nguzo za umeme yaan zile nyaya unaziona hizi hapa usoni basi ukizikaribia unainama aiseešŸ˜€
 
Usinikumbushe mkuu. Miaka ya 90s kuelekea 2000 huo ulevi ulikuwa kama fasheni kwa vijana.

Siku hiyo nikaenda kununua. Mimi na mjomba wangu tukaijaribu. Ebhana weee!!. Kila mtu aliinama kasizi kwenye kona yake kwa kama dakika 30 bila kutikisika. Kichwa kizito, unatamani kukaa na kulala kwa muda mmoja.

Usikute sababu ya kupigwa marufuku kuna viongozi wasiotaka kilevi kiwapite mbele yao wakaijaribu. Nao wakaona mziki wake. Wakaona mhh!!, hii siyo.
 
Kuiona tu hiyo pakti imenifanya kichwa kianze kuniuma kwasababu ni mojawapi ya memory mbaya niliyonayo, ilichonifanya sitasahau.
Nilibwia nyingi na papo hapo nikanywa viroba kipindi hicho vilikuwa maarufu Sana nimesahau jina aisee nashukuru Mungu alininusuru sikukata Moto ila Ile ilikuwa inanipeleka.
SITASAHAU NA TANGU HAPO NILIAPA SITAKUJA KUNYWA POMBE WALA KILEVI CHOCHOTE NA KWELI SIJAWAHI.
 
Kuber hiyo..šŸ˜‚šŸ˜‚
Kuna bibi mmoja alikua anaitwa bibi’ake Suma kila ikifika jioni ananiagiza duka moja maarufu siwezi kulitaja nitafungua codešŸ˜‚

Sasa mambo ya utoto utoto nikaona anafaidi… siku nikaipasua kidogo nikachota nikamimina kama navyomuona aalivyokua anafanya..

Nilikimbizwa hospitali ya mnazi mmoja šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚ nilijinyeaaa sitasahau kudadekišŸ˜‚šŸ˜‚
 
Hahaaaaa hatari sana..
Nilikuwa nashinda kijiweni na masela wanatumia kila aina ya kilevi.
Siku moja nami nikagongea hii kitu...
Kwakweli dakika 5 zilikuwa nyingi, kizunguzungu, jasho mwili mzima yaani sijielewi kabisa.
Nilijikimbiza home nikanywa maziwa fresh nilitapika vya kutosha, nikapiga usingizi wa maana.
Sikurudia tena.
 
Mwaka 2001 Nilikuwa na Demu wangu sijui kama anatumia hiyo kitu.. Sasa msimu wa likizo kuna siku nikaenda kwao.. Nikashinda naye.. Kumbe alikuwa na alosto akawa hataki nijue anatumia Kuber.. Akawa kakausha.

Basi mimi sijui nikaaga nikasepa kama dk tano nikagundua nimesahau simu yangu kuifuata nakuta demu mdomo mzito. Nikamuliza vipi tena Asee akani onesha pakti akanambia anabwia..

Basi Nakumbuka kesho yake nili msindikiza mgeni apande treni.. Pale stesheni Si nika uona Nakumbuka ulikuwa unauzwa Jero nika nunua, nikaifungua ile harufu yake kama karafuu nika ichukulia powa.. Nika ibwia kama yote.. Thubutuuu.....

Sitasahu hiyo siku.. Nilitokwa Jasho nilijamba.. Nili nyong'onyea, Mwili ukakosa nguvu.. Ilibidi nika harishe.. Kwanza.. Baada ya hapo Nilikuwa nikiiyona hiyo pakti natapika..
2001 hukuwa na umri was kujielewa.Umefurahisha kijiwe tu. Et umesahau simu nyumbani kwa demu wako 🤣🤣 wakati huo simu sio kitu cha kila mtu anayo. Then unasema 500 kuber!!! Unaijua mia 5 ya mwaka 2000?? Kumbuka mtoto wa kishuaa ndio anaenda shule na 50. Hapo ananunua embe la kukata sh 10 au zima sh 30. İnaweza kupata maji ya kifuko sh 5, ubuyu sh 5,muhogo sh 5. Tumenunua sana Kuber kwa hela za shule haikufika jero. Bia yenyewe haikuuzwa jero mwaka 2000
 
Back
Top Bottom