Katika bara zima la Afrika, vijana sio tu wamekuwa washiriki, bali ni sehemu muhimu ya kuongeza kasi ya mageuzi ya bara hilo. Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika, bara hilo ni makazi ya idadi kubwa ya vijana duniani, likiwa na zaidi ya watu milioni 400 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 35, na idadi ya vijana katika bara hilo inatarajiwa kuzidi milioni 830 itakapofika mwaka 2050.
Hali hiyo, ikichochewa na mageuzi ya kidijitali na mabadiliko yake kuelekea nishati ya kijani, inafungua fursa nyingi mpya kwa vijana wa bara hilo. Kwa kushirikiana na wenzi wa kimataifa kama China, nchi za Afrika zinatumia fursa hii kuwawezesha vijana wake kuunda hatma nzuri zaidi na za kiuvumbuzi.
Kwa mujibu wa jukwaa la Statista, idadi ya jumla ya watu barani Afrika inazidi bilioni 1.46 mpaka kufikia mwaka 2023, na inatarajiwa kufikia watu bilioni 2.5 itakapofika mwaka 2050. Katika “Waraka Mweupe wa AI na Kazi za Baadaye barani Afrika,” kampuni ya Microsoft inakadiria kuwa mpaka kufikia mwisho wa karne ya 21, Afrika itakuwa makazi ya karibu nusu ya vijana wote duniani, ikiwa ni karibu mara mbili ya idadi nzima ya watu katika bara la Ulaya.
Uwepo wa nguvukazi kubwa ya vijana kunaleta uhai katika sekta za jadi kama kilimo, viwanda na huduma, huku kukiongeza kasi ya maendeleo ya sekta zinazoibuka kama uchumi wa kidijitali, nishati mbadala na Akili Mnemba (AI). Pia, kizazi hiki cha vijana kinatumika kama nguvu kubwa ya watumiaji, na kuchangia katika ukuaji wa kivutio cha soko la Afrika.
Katika ripoti yake inayoitwa “Mwenendo wa Ajira Duniani kwa Vijana mwaka 2024,” Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) limesema idadi kubwa ya vijana barani Afrika inaweza kuthibitika kuwa ni mali ya thamani kubwa kwa bara hilo katika kuendelea mbele wakati maeneo mengine duniani yakikabiliwa na idadi kubwa ya wazee na uhaba wa nguvukazi.
Katika kampuni ya chai ya mitishamba ya Yaxare iliyoko katika mji mkuu wa Gambia, Banjul, mwanzilishi wa kampuni hiyo, Fatoumata Njie anasimamia ufungishaji wa bidhaa zake, ambazo zimepata umaarufu kwa wateja wa ndani kutokana na mwingiliano wa teknolojia ya kidijitali katila usimamizi wa biashara yake. Ili kuboresha ybora na mavuno ya dawa za mitishamba za huko, Njie ametengeneza APP ya simu inayoitwa “Happy Farm,” inayowasaidia wakulima kuongeza ubora wa udongo na kuongeza mavuno. Wakati huohuo, mara kwa mara anaagiza vifaa vya kuchakata na kufungashia chai kutoka kwenye majukwaa ya biashara ya mtandaoni ili kuwapatia wateja wake bidhaa zinazovutia na zenye ubora wa juu.
Kutokana na mageuzi ya kidijitali, maisha ya kila siku ya vijana wengi barani Afrika kama Njie yanapitia mabadiliko makubwa. Katika bara hilo, biashara za mtandaoni na fedha za kidijitali zinapiga hatua kubwa, huku malipo kwa kutumia simu za mkononi pia yakiendelea kupata umaarufu. Wakati miundombinu ya mawasiliano ikiendelea kuboreshwa, kazi mpya na fursa mpya za ujasiriamali zinazidi kuongezeka kwa vijana wa barani Afrika.
Karakana ya Luban ni moja ya ushirikiano wa China na Afrika katika elimu ya vijana. Katika miaka mitatu ijayo, China itaendelea kutekeleza Hatma ya Afrika, mradi wa ushirikiano wa China na Afrika katika elimu ya ufundistadi, kujenga shule za teknolojia ya uhandisi na nchi za Afrika, kuanzisha ama kuboresha Karakana za Luban na shule 20, na kutoa fursa za mafunzo ya miradi inayolenga maendeleo ya vijana.
Nchi za Afrika pia zinafanya juhusi kuwawezesha vijana kupitia miradi maalum ya maendeleo, mfano ukiwa ni mpango wa serikali ya Morocco wa kuwekeza dola za kimarekani bilioni 1.4 kwa ajira za vijana, Programu ya Maendeleo ya Vijana ya Senegal ya mwaka 2025 – 2029, na miradi ya mafunzo ya kidijitali ya Zambia itakayomalizika mwaka 2027.