Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Kajiridhishe. Maana hao wote wanoingia kwenye kutalii chuga wengi hupotia airpot ya dar
Dar ni exit gate kwa watalii wanaotokea kaskazini.
Iko ivi KIA - kilimanjaro, ngorongoro, serengeti anapanda pipa kuelekea zanzibar or Dar kurudi nyumbani.
Watalii wanaopitia dar mara nyingi n selou,sadan au bagamoyo to zanzibar or back home mara chache wanaopitia huko kuja kaskazini.
Mnatulaumu sanaa na lifestyle letu ila si tunaona poa tu maana hata sisi tunachoshwa na masalamu mengi,na ndio utamu wa kuwa na mikoa mingi yenye lifestyles tofautitofauti.
Niko so proud kuzaliwa,kukulia Arusha.
 
Arusha wanaushamba mwingiii ila wao wanajiona ndio wajanja, hawana tofauti na wahuni waliozaliwa na kukulia ilala ambao hawajui maeneo mengine TZ

Nb: hivi kile kiswahili cha Dar mbona kuna watu maarufu waliokulia huko mfano Diamond ,manara hatuwasikii wakikiongea?

Vilevile kina Nikki hawana kile kiswahili cha usela mavi cha Arusha
 
Nimetoka huku ukweni juzi tu,wife alifiwa na kaka yake..Daah kwa yale niliyoyashudia hiyo wiki niliyokaa itoshe kusema hakuna vijana wa hovyo na wapumbavu wenye usela mavi kama vijana wa Arusha mjini( huko wilayani angalau kuna unafuu) jamii ile ina ishi kiwasi wasi sana muda wowote huisi wanaibiwa au wanataka kudhuriwa ....

Maduka mengi jion wanajaa vijana wanakunywa ma k- vant na stori za kipumbavu...kiingereza kingi na ufala mwingi eti wanajidai wasomi wanaishi kihuni .

Wanasubiri ukienda dukani wakupige mzinga...

Ndio maana nimejua kwa nin wife hatakagi watoto likizo wasikae wiki huko arusha kwao...
 
Kwa hiyo yupi mjanjanja zaidi ya mwenzie!!?? Mchaga au Mchugaa!!??
Mchagga, Mwarusha, Mmeru sionagi tofauti yao kuanzia kuongea, lifestyle na hata fighting

Wana Roho ya Uthubutu, ubabe ubabe n.k tofauti na makabila mengine....ni kama Wakikuyu wa Kenya

Wanawaza pesa na starehe tu

Hata Dada zao Wanafanana tu
 
Nimetoka huku ukweni juzi tu,wife alifiwa na kaka yake..Daah kwa yale niliyoyashudia hiyo wiki niliyokaa itoshe kusema hakuna vijana wa hovyo na wapumbavu wenye usela mavi kama vijana wa Arusha mjini( huko wilayani angalau kuna unafuu) jamii ile ina ishi kiwasi wasi sana muda wowote huisi wanaibiwa au wanataka kudhuriwa ....

Maduka mengi jion wanajaa vijana wanakunywa ma k- vant na stori za kipumbavu...kiingereza kingi na ufala mwingi eti wanajidai wasomi wanaishi kihuni .

Wanasubiri ukienda dukani wakupige mzinga...

Ndio maana nimejua kwa nin wife hatakagi watoto likizo wasikae wiki huko arusha kwao...
Mawazo sasa inabidi yabadirike apa
 
Kuna siku nlipishana na machalii wawili mida ya saa tatu usiku, mitaa ya pale mianzini, wakiwa na umri kati ya miaka 13 au 14 hivi.

Mmoja kiunoni anabonge la beto, anamwambia mwenzake "haki ya mama, yule manzi asingetoa ile simu, mi ningemvurugua maini asee".
Beto ni nini? Nyie watu wa Arusha uhuni sio ujanja
 
Mwanadam hasikii asichoelewa ndio maana wewe unaona ni lifestyle mbaya wao wanaona ni ujanja ,kama vile wachawi wewe utaona ni ujinga kuacha mambo yako ukaanze kuroga watu ila wachawi wao wanaona kwao ni ujanja na wanaenjoi tu, maisha ndivyo yalivyo .
 
Arusha inahitaji wokovu wa Programu maalum ya Kisayansi kuwatoa walipo. Hali ya Usalama pia siyo ya 100% vijana wamevurugwa ubongo muda wowote anakutoa uhai. Arusha siyo mahali sahihi kulelea familia kuna tatizo la jumla kwenye ile jamii
Sio salama kabisa, wiki iliyopita nilifika Arusha saa sita usiku pale stand.Aisee inahitaji ujitoe ufahamu na uwe imara sn ktk kujilinda na kulinda mzigo wako.Yani vijana wanaona mizigo ya kwenye buti ni yao vile wanakuzuia mwenye mzigo kuchukua. Ilibidi abiria tulioshuka kwenye gari tuungane tuwe wakali na kuonya asisogee mtu.Kuna kitoto kiliniangalia vibaya kwasababu nilikisukuma.

Nikakiita,nikasema nitakuchuna ngozi,sisi watu wa Mbeya huwa tunachuna ngozi na kuchukua ulimi,kikaogopa kikapotea mazingira yale.
 
Mchagga, Mwarusha, Mmeru sionagi tofauti yao kuanzia kuongea, lifestyle na hata fighting

Wana Roho ya Uthubutu, ubabe ubabe n.k tofauti na makabila mengine....ni kama Wakikuyu wa Kenya

Wanawaza pesa na starehe tu

Hata Dada zao Wanafanana tu

We fala-eli unataka tuwaze nini ? Ujinga kama mlivyo makabila mengine, umaskini mpaka kwenye kope
 
Mtoa mada ungejua sisi tuko mbele kuliko nyie, muulize nyerere kwanini alitusii tusiwe nchi nyingine. Sisi tulidai uhuru wa nchi yetu Arusha kama yote bro. Tunawaburza kila kona ya maendeleo. Usituone powa mzee
 
View attachment 2707633

Kunahitajika PROGRAMU ya dharura kuliokoa hili jiji.

Sina maana ya kusema vijana wote wa Arusha ni wahuni na waalifu ama kusema Arusha si salama kabisa, La Hasha! ni kwamba uhuni ni kama umefumbiwa macho usambae mithiri ya kansa ya kidole inavyosambaa mwilini kwahio sio jambo la kufumbia macho kwamba eti kwasababu sio wote basi wapuuziwe, kumbuka hata mayai machache yaliyooza yatazidi kuozesha mengine hatua zisipochukuliwa, kwa wale tuliosoma soma nadhani tunajua kitu kinaitwa compounding.

Vijana wengi ni waliozaliwa na kukulia hapa hapa ni jamii za wazawa wenye asili ya Arusha kama Wameru na Waarusha pamoja na jamii za wenyeji ambao walihamia na wapo kwa muda mrefu kama Warangi, Wachaga, Wambulu, Wanyaturu.


Huu utamaduni wa kutukuza uhuni sijui ulifika vipi huu mkoa lakini unazidi kuleta athari kubwa, ulianza kidogo ila unazidi kukuzwa na kufanywa na vijana wengi wa sasa walioukuta tangu wakiwa wadogo, Mazingira ya jamii inayowazunguka na Mifumo ya malezi imekuwa mstari wa mbele kuwa kichocheo.

Kijana akiwa mhuni ama muhalifu ni jambo analoweza kujisifia na kupewa heshima, akienda jela ni kama cheo kabisa kisicho na shaka kwamba aliwahi kupiga tukio.

mapikipiki haya yanakimbizwa vibaya mno ili tu kupata sifa, vijana wanapoteza maisha kwa sifa za muda mfupi, tena sikuhizi kumezuka makundi ya kuendesha kwa kuinua tairi, Mbaya zaidi hawavai uniform za kujilinda ama kutumia pikipiki maalum za michezo, wanatumia bodaboda hizi za kichina za kubebea abiria na hapo hana jaketi gumu, hana kiatu kigumu kirefu, hana begi la sponji kulinda mgongo, hajavaa gloves za mikono, hana guard za viwiko na makoti, hana hata helmet kavaa mzula wa baridi ila anadiriki kuendesha kwa kasi ama / na kunyanyua tairi la pikipiki isiyo ya michezo, ajali hizi za kujitakia zipo nyingi vijana wanazikwa kama kumbikumbi, wengine wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika....

vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi, sina shida na matumizi ya vilevi hata mimi ni mdau ila nafata misingi,tatizo makundi yanaponza sana na kuchangia abuse (abnormal use), wanatumia kwa kuigana au ile kutaka kuonekana wamepinda ili kupata uhakiki kutoka wenzao kwamba ni wajanja, na ndio hapa mtu ananasa kwenye uraibu.

Kuna Umakundi makundi wa kihuni huni wanaoishi bila future,

Suala la kupigana beto (visu) nalo halipo nyuma, Sime na visu vimekuwa vitu ambavyo vinazidi kuzoeleka kutumika sio tu kwenye uporaji bali hata kwenye ugomvi , niliwahi shuhudia live kwa macho yangu pale karibu na stendi ugomvi niliodhani watu watachapana ngumi niliona mtu anapigwa kisu damu inamwagika, hata wasanii wa huko kina Lord Eyes na Fido Vato wamewahi kupigwa visu,Marehemu Father Nelly wa kundi la X Plastaz aliuliwa kwa visu.

Wizi nao hauna dalili ya kupungua, watu wanaporwa kikatili sana inabidi utii amri lasivyo utavurugwa maini na beto, bodaboda wanaibiwa pikipiki mpaka kuuwawa, ujambazi nao upo wa kuvamia matajiri, kwa ufupi kuna famjlia zinajulikana kabisa wanaishi mjini kwa shughuli hizo lakini ndio wanapewa heshima maana uhuni unaonekana ujanja.

Suala la maadili nalo limepungua sana na hii imechangia sana hata makanisani na misikitini kuwepo na upungufu mkubwa sana wa vijana,
Kuna msiba vijana wameshiriki mazishi ya mwenzao mara wakataka mchapa mchungaji kisa mchungaji aliwapa maneno ya kweli wakachukua maiti kwenda kuizika wenyewe, kuongea hovyo hata mbele ya camera mpaka hivi sasa imekuwa kama jadi yao, mavazi wanayoona yanayomwakilisha mwana arusha original ni kuvaa mashati marefu mpaka magotini pamoja na miviatu mikubwa kuliko size za miguu.

Ajabu ni kwamba hata polisi ni kama vile wamefumbia jicho ama jitihada wanazofanya ni ndogo sana, ni kama vile wamezila na kujikatia tamaa wamewaacha wenye mji wafanye watachojua wao with little interference
Bora kuwa mkoa WA kihuni.. kuliko WA kichoko[emoji1787]
 
Sijawai fika Arusha.. But nimepata kitu.. next holiday ntatembelea hapo ila naomba mwenyeji kama upo tuwasiliane nikujue
 
Back
Top Bottom