View attachment 2707633
Kunahitajika PROGRAMU ya dharura kuliokoa hili jiji
Vijana wengi wahuni ni wazawa wa hapa hapa Arusha na matokeo ya kuukuta utamaduni wa kutukuza uhuni tangu wakiwa wadogo, imeshakuwa ndani ya mfumo wa maisha wa vijana wengi kwamba ili uonekane mjanja basi uwe mhuni wa kunywa pombe kali, kuvuta bangi ama uwe mhalifu.
mapikipiki haya ya wanakimbiza vibaya mno, ajali kila siku, wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika miguu,.Bodaboda za kutaftia riziki wanalazimisha ziwe pikipiki za michezo, ukienda kwenye magroup yao haya ya kudandia pikipiki kuna "pumzika kwa amani / rip" nyingi sana.
vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi, sina shida na matumizi ya vilevi ila wao wanavitumia kupita kiasi.
Makundi ya vijana wengi ni magenge ya vijana wanaoishi bila future, wanafanya vingi bila kujali madhara wala kesho.
Suala la kupigana beto (visu) nalo halipo nyuma, Sime na visu vimekuwa vitu ambavyo vinazidi kuzoeleka kutumika sio tu kwenye uporaji bali hata kwenye mabifu ama ugomvi baina ya vijana, nilikua naangalia clip moja hata msanii wa huko anauvuma kwa sasa Fidovato analalamika vijana wanapigana sana beto.
Wizi nao hauna dalili ya kupungua, watu wanaporwa kikatili sana inabidi utii amri lasivyo utavurugwa maini na beto, bodaboda wanaibiwa pikipiki mpaka kuuwawa, ujambazi nao upo wa kuvamia matajiri, kwa ufupi kuna famjlia zinajulikana kabisa wanaishi mjini kwa shughuli hizo lakini ndio wanapewa heshima maana uhuni unaonekana ujanja.
Ajabu ni kwamba hata polisi ni kama vile wamefumbia jicho ama jitihada wanazofanya ni ndogo sana, ni kama vile wamezila na kujikatia tamaa wamewaacha wenye mji wafanye watachojua wao with little interference