Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

'Peer groups' inawaponza vijana, wengi hufanya hayo kwa kuiga tu ili kuonekana 'wamepinda'.
 
Arusha umeishi wapi au umekulia wapi unaijua Arusha wewe

We fala, mimi nimezaliwa ngarenaro, na ili niende shule napita matejoo natokea Majengo.

Chocho zote nazijua, kuanzia esso, unga limited, lemara, mianzini, kila mahali.

Katika kila kituo cha boda kuna kiongozi, na kuna watu wazima wengi sana wenye busara.

Uhuni upo, sio kwa kiwango cha kusema kuba tataizo, Arusha hakuna shida ya wahuni, ni ujinga na mtazamo.
 
Elezea tena umejichanganya nimekuuliza umeishi wapi na umekulia wapi sijakuuliza umepita chocho zipi
 
💯
 
Vijana wa huko wengi washamba sana na hawajiamini mpaka waboost na bangi na kupenda uhuni wa makundi ,ukiwatoa nje ya hapo kama samaki katolewa kweny maji.

Wengi ni washamba wanaishi maisha ya miaka 80's kuanzia mavazi yaani ukipita hapo utaona watu wamevaa nguo za zamani ..Bado mjini mtu anavaa makatambuga Yale ya wamasai kuchungia.
 
Arusha inahitaji wokovu wa Programu maalum ya Kisayansi kuwatoa walipo. Hali ya Usalama pia siyo ya 100% vijana wamevurugwa ubongo muda wowote anakutoa uhai. Arusha siyo mahali sahihi kulelea familia kuna tatizo la jumla kwenye ile jamii

Arusha si sehemu sahihi ya kulea familia?
Unapotosha hapo, umeandika as if arusha nzima mbaya wkt ni maeneo machache na si aarusha nzima.

Watu wamezaliwa na kukulia mpaka kazi na wapo na hawajageuka wahuni.

Ni sawa na kusema dar nzima ni mashoga au wauza unga, wkt ni maeneo machache.
 
Arusha nadhani ndio Mkoa wanaongoza kwa kutukana hadharani matusi na hata hawajali harafu wakiwa wanaendesha gari binadamu yeyote anaetembea kwa mguu wanamuona kama ng'ombe tuu wengi hawajali hata kuwapa fair watoto wa shule au gari inayoingia bara bara kubwa...
Wazulu hawajatofautiana sana na watu wanaoishi Arusha wana tabia za ajabu ajabu sana harafu wakimuona mtu ana Vipesa pesa kidogo wanamnyenyekea na kumwita Fogo hapo ukute ana Viford (Hiace) vyake viwili vinaenda kwa Mromboo mjini na akiweza kuwanunulia Gomba wachanje ndio balaa zaidi...
 
Its not government's job to regulate morality
 
Yupo sahihi acha usela mavi dogo. Kama wanataka waishi maisha yao wasikate na kujeruhi wengine. Akishalewa viroba vyake akiwa na hamu ya kuchoma mtu kisu, ajichome cha tumbo na sio kujeruhi wengine.
Sawa bana chalii ya dar!
Huijui chuga wewe unangaliia ma clip ya Facebook huko!
Wivu tu umewajaa na jiji letu ndo maana mnalialia
 
Ni ujinga na ulimbukeni tu wa washikaji wanaotoka maisha duni. Ila Arusha ukiwa na akili iliyotulia unatoboa life.

Ni kweli ushindani ni mkubwa na waliokata tamaa ndio wamekuwa na uhuni wa kijinga.

Kuna mitaa kizazi kinapotea sana, inasikitisha.
Wakiona vile vituko badala kusikitika wanasema "Arusha iwe nchi bhana" yaani piga hesabu ndo mwanao anakuwa wa hovyo kuvaa manguo oversize na bangi nyingi🥹.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…