Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Sio salama kabisa, wiki iliyopita nilifika Arusha saa sita usiku pale stand.Aisee inahitaji ujitoe ufahamu na uwe imara sn ktk kujilinda na kulinda mzigo wako.Yani vijana wanaona mizigo ya kwenye buti ni yao vile wanakuzuia mwenye mzigo kuchukua. Ilibidi abiria tulioshuka kwenye gari tuungane tuwe wakali na kuonya asisogee mtu.Kuna kitoto kiliniangalia vibaya kwasababu nilikisukuma.

Nikakiita,nikasema nitakuchuna ngozi,sisi watu wa Mbeya huwa tunachuna ngozi na kuchukua ulimi,kikaogopa kikapotea mazingira yale.

[emoji1787]
 
Niliwahi lisema hili kwenye kundi la marafiki zangu wengi wapo Arusha wakaanza kuniambia nilete hayo matukio ya kijinga wanayoyafanya. Ishu ni kwamba hata watu wenye akili zao wanashadadia huo ujinga bila kujua ndo wanaangamiza taifa na kizazi hiki, mwisho wa siku utasikia wakiwapa lawama serikali. Serikali inaanzia nyumbani na kwenye jamii inayokuzunguka. Kama jamii ni ya wezi huwezi pata kiongozi asiye mwizi kama jamii ni ya kihuni hata viongozi nao watakua ni walewale tusimame wote kidete kupinga huu ujinga.
 
NIlipata kazi Arusha kwenye ofisi za shirika fulani, nilienda kuripoti na kusoma mazingira ili nione kama naweza hamishia familia, baada ya wiki nilirudi zangu Dar na kazi nikaacha maana niliona mazingira sio rafiki kwa malezi na usalama wa watoto, mpaka na leo napachukia Arusha sitamani hata kwenda kutembea
Naomba ukipata muda ujibu
Uliona nini cha ajabu Arusha mpaka ukakayaa kufanya kazi maana naona lawama zinarushwa tu ila hamna sababu ya msingi
Au nawewe ulipita hukusalimiwa?

Arusha haina muda wa umbea jomba
Nani ahangaike na hako kamaisha kako

Watu wa mikoa mnataka mkifika mahali mpewe recognition afu watu unakuta wapo bize na maeeee yao
 
Naomba ukipata muda ujibu
Uliona nini cha ajabu Arusha mpaka ukakayaa kufanya kazi maana naona lawama zinarushwa tu ila hamna sababu ya msingi
Au nawewe ulipita hukusalimiwa?

Arusha haina muda wa umbea jomba
Nani ahangaike na hako kamaisha kako

Watu wa mikoa mnataka mkifika mahali mpewe recognition afu watu unakuta wapo bize na maeeee yao
😆😆😆 walinitolea kisu mchana peupe jomba na kuna watu barabarani wakaniambia achia mkoba

Thangu hiyo siku nikajikuta naona Arusha hakuna usalama
 
Back
Top Bottom