Vijana wa Bongo jifunzeni kwa CR 7

Vijana wa Bongo jifunzeni kwa CR 7

Mbona Numbisa amejibu vyema hoja ya mleta uzi.

Mleta uzi anajaribu kumtumia Ronaldo kama mfano kwa vijana wa Bongo na wasanii baadhi yao ambao wamekuwa wakiwasema baba zao vibaya.

Numbisa anasema Ronaldo hakuwahi kukataliwa au kutelekezwa na baba yake na hili ni kweli, au labda kama wewe una habari nyingine za CR7 kukataliwa na baba yake?

Katika mazingira kama hayo huwezi kumtumia CR7 kama mfano kwa vijana ambao walikataliwa na wazazi wao na hata kutelekezwa.

Mkuu, hakuna mtu anaweza kumpandikiza chuki mtoto wako kama wewe utakuwa nae wakati wote na yeye akakuona.

Wanaume tuache ujinga, tulee watoto wetu. Acheni ujinga na upumbavu wa kuwasingizia wanawake eti wanawajaza watoto chuki. Mtoto atakuchukia tu kama wewe ni mjinga ulimimina mbegu na ukakimbia, hukumtunza unataka akupende?
Huwajui wanawake wabongo wew utatunza utamlea ila ukijikwaa mkagombana nahuyo mzaz mwenzio haijalishi nimkeo au mchepuko chuki anazihamishia kwamtoto
 
Funzo tunalolipata hapa Kwa Huyu Mwamba CR7 ni kwamba 'Usizae hovyo hovyo' nje Ya ndoa halafu Na Usitelekeze Mtoto mpaka afikie hatua Ya kulishwa Matango pori Na Mama Yake...!

Sasa nyie Vijana Endeleeni Na Kampeni Yenu ya Kishetani huku Mkibana pua 'Kataa ndoa'..... Sijui Mnataka kujiunga Na Wale Wa Upinde?
Kwakuwa umetugusa acha tukujibu.
Migogoro mingi ya wazazi huwa inaanzia kwenye ndoa na mwisho wa siku mwanamke hutumia fursa yake ya kushinda na watoto muda mwingi kuwalisha sumu juu ya baba yao.
Ukichunguza kwa kina wanaume wengi wenye watoto bila ndoa huwa ni wawajibikaji na hawana muda wa malumbano na wazazi wenza. Tengenezeni vzr mazingira ya ndoa zenu badala ya kumalizia stress kwetu tusio na ndoa na tusiohitaji kuoa.
#KATAANDOA
 
Usitake kupingana na ukweli... hoja yako ya Ronaldo kutokukimbiwa au kukimbiwa na Baba haina mashiko Dada.

watasha hawanaga huo ujinga wa kuwapandikiza watoto chuki kama nyie wanawake wa kiafrika.

Ikiwa ukweli ataweka ukweli wazi na ikiwa uongo atauweka wazi.

Baba yake na Ronaldo alikuwa mlevi au mraibu wa pombe kupita maelezo mpaka kuna muda alishindwa kufanya kazi na kuendesha familia. Jukumu alilishika Mama yake na baadhi ya kaka zake. Lakini hata siku moja huyo bwana hajawahi kusimama na kumkana au kumkashifu baba yake. Wala mama yake hawezi kuruhusu hilo.

Sio huyo tu wapo wachezaji wengine wana historia ngumu na rafu sana za maisha ya utoto kama vile Ibrahimovic lakini hakuna anayejua na wala hasimami kumponda baba yake. Tazama waafrika sasa 😅


Usitetee upuuzi! Muache kupandikiza watoto chuki na kuwarithisha ujinga wenu.
Bongo unakuta wanawakata baba zao halafu wanaongozana na mama zao kila mahali utafikiri hao mama zao ni madem wao wapya
 
Huwajui wanawake wabongo wew utatunza utamlea ila ukijikwaa mkagombana nahuyo mzaz mwenzio haijalishi nimkeo au mchepuko chuki anazihamishia kwamtoto
Ukitafuta sababu za kutomlea mtoto wako utazipata, ni nyingi sana lakini nakuhakikishia kwamba zote ni za kijinga.

Nimekuwa hapo mkuu, nimelea mtoto na mwanamke katika mazingira hayo. Hata ukigombana na mwanamke usikubali yeye amuingize mtoto kwenye ugomvi wenu. Tatizo kubwa kwetu wanaume, ukikosana na huyo mzazi mwenzio unamsusa na mtoto na hapo ndio mtoto anaanza kulishwa sumu. Hakuna mahusiano kati yako na mtu uliyezaa nae ukiachana na kumlea mtoto.
 
Funzo tunalolipata hapa Kwa Huyu Mwamba CR7 ni kwamba 'Usizae hovyo hovyo' nje Ya ndoa halafu Na Usitelekeze Mtoto mpaka afikie hatua Ya kulishwa Matango pori Na Mama Yake...!

Sasa nyie Vijana Endeleeni Na Kampeni Yenu ya Kishetani huku Mkibana pua 'Kataa ndoa'..... Sijui Mnataka kujiunga Na Wale Wa Upinde?
Kwani cr7 kaoa?
 
Back
Top Bottom