Kambi nyingi za Jeshi ktk nchi zetu hizi za dunia ya tatu ambazo nyingi zinafuata mfumo wa kikomunisti au ujamaa (udikteta) utagundua kwamba ni kama Kambi za Mateso (Tourture Centers or tourture camps) badala ya kuwa kambi ambazo watu wachukua ujuzi na maarifa ya kijeshi, wakati kambi za Jeshi ktk nchi zingine ambazo zinafata mfumo wa nchi za Magharibi wa kiliberali utagundua kuwa ni Kambi za Mafunzo ya ujuzi na umahiri ktk masuala ya kijeshi, zinalenga ktk kujenga umahiri (competence) ktk nyanza zote za kijeshi.
Mfano mdogo tu kuthibitisha hoja yangu hii, rejea tukio la majibizano ya risasi kati ya Hamza Mohamed na wale Mapolisi wengi waliokwenda kumdhibiti pale Selander bridge. Ukichunguza kwa umakini mkubwa zile video zinazoonyesha jinsi Askari Polisi walivyokuwa wanapiga risasi kuelekeza kwa Hamza Mohamed na jinsi Hamza alivyokuwa aki-react dhidi yao hao Polisi utaona ushahidi wa hicho nilichosema.